Pages

Pages

Thursday, March 14, 2013

Wazee wa Ngwasuma nao kutua leo Garden Breeze, Magomeni



Rais wa FM Academia, Nyosh El Sadaat

Na Kambi Mbwana, Dar es Saalam
RAIS wa FM Academia, Nyosh El Sadaat, amesema kwamba wamekubali kufanya shoo kuanzia Ijumaa hii katika viwanja vya Garden Breeze, Magomeni, ili kuweka ukaribu na uhusiano mzuri na mashabiki wao bila kubagua uwezo wao.


Shoo ya Garden Breeze hufanyika bure na kushirikisha watu wengi wanaojaa katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuburudika na muziki wa dansi hapa nchini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Nyosh alisema kuwa awali waliweka ngumu kufanya shoo kwenye viwanja hivyo, lakini baada ya kuzungumza na wadau wao, wakaona si vyema kuendelea kugoma.

“Hii ni nafasi ambayo kwakweli wadau walikuwa wakiangalia namna gani sisi tutakuwa wagumu kukubali kufanya shoo katika viwanja hivyo vya Garden Breeze.

“Lakini nashukuru kuwa tumefikia wakati muafaka kwa kuhakikisha kuwa kwa pamoja tunaangusha shoo ya aina yake katika viwanja hivyo kuanzia Ijumaa hii,” alisema.

Kwa kukubali kufanya shoo katika viwanja vya Garden Breeze, FM Academia sasa itakuwa sambamba na wakali wengine, Extra Bongo, Mashauzi Classic, Msondo Ngoma na bendi nyingine zinazofanya shoo katika viwanja hivyo.

No comments:

Post a Comment