Pages

Pages

Thursday, March 14, 2013

Nashukuru kwa kuniunga mkono na leo siku yangu ya kuzaliwa



                             Kambi Mbwana

MUNGU ANANIPENDA NA ANAKUPENDA PIA
LEO ni siku yangu ya kuzaliwa baada ya kutimiza miaka 29 ya kuzaliwa kwangu, katika kijiji cha Komsala, wilayani Handeni mkoani Tanga.

Namshukuru Mungu kwa kunileta kwake duniani, sambamba na wazazi wangu, Mbwana Hemed na mama yangu Fatuma Rashidi kwa kunivumilia hadi leo najitambua.

Wakati naifurahia siku hii, nawashukuru wote waliochangia kwa namna moja ama nyingine katika maisha yangu, maana kuna wakati tulikwaluana, ila tulikaa na kuyamaliza kibinadamu.

Nawashukuru na muendelee kuniunga mkono katika kila jambo ninalofanya, ikiwamo blog yako ya Handeni Kwetu. Aidha, nikiwa kama binadamu sitakatai kuchukiwa na anayependa hivyo, ila asinichukie bila sababu za msingi, hivyo kwenye makosa naomba nisemwe au kuelekezwa pia.

Nachukua fursa hii kuwashukuru wooote mliotumia muda wenu na kuni wish leo siku yangu ya kuzaliwa. Mungu awabariki woooote kila mmoja kwa nafasi yake maana ni wengi na wameonyesha upendo wa kweli kwangu?

SWALI: Kwani mimi ni nani? Na hao pia ni nani? Tumekuja duniani kufanya nini? Je, wewe unaweza kunielezea kuwa ni nani? Majibu nijuze kwenye in box au vyovyote upendavyo. ASANTE MUNGU MUUMBA MBINGU NA ARDHI.

No comments:

Post a Comment