Pages

Pages

Wednesday, March 13, 2013

GODBLESS LEMA AITISHA MAANDAMANO

 


Lema aitisha maandamano
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, pichani, ametangaza kuandaa maandamano makubwa yatakayoshirikisha wanawake na watoto katika Jiji la Arusha ili kushinikiza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA) kuwasambazia maji.

Akizungumza jana, Lema alisema ameamua kuandaa maandamano hayo ya kudai maji kwani kwa zaidi ya miezi sita sasa asilimia 70 ya wakazi wa Jiji la Arusha hawapati maji safi.
“Nimewaandikia barua AUWSA wiki mbili sasa nikiwataka wanipe mipango yao ya muda mfupi na mrefu ya kuondoa tatizo la maji Arusha, kwani mimi kama mbunge ninaweza kushirikiana nao kupunguza tatizo hili, lakini hawajajibu sasa tutawashinikiza kwa nguvu wa umma,” alisema Lema.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa AUWSA, Mhandisi Ruth Koya hakupatikana kuelezea kama amepokea barua hiyo baada ya kutopatikana ofisini, pia simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani.

No comments:

Post a Comment