Pages

Pages

Saturday, March 16, 2013

Walimu 152 waripoti wilayani Kilwa kwa ajili ya kutumikia ajira zao


Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa akiwakaribisha walimu wapya

Na Mwandishi Wetu, Kilwa
JUMLA ya walimu wapya 152 wa shule za Msingi na Sekondari wameripoti wilayani Kilwa kati ya walimu 182 waliopangwa kufundisha Wilayani humo. Akizungumza kwenye mkutano na walimu hao Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega alisema walimu walipangiwa kufundiosha Wilayani humo walikuwa ni 182 kati ya hao 104 wa Shule za Msingi na 78 wa Sekondari.


Aidha Ulega alifafanua kuwa walimu wasioripoti licha ya muda wakufanya hivyo kumalizika ni 7 wa Shule za Msingi na 23 wa Sekondari. Tukio hilo la kuwapokea walimu hao limekwenda sambamba na makabidhiyano ya meza nne za maabara inayotembea kwa ajili ya mafunzo ya vitendo katika masomo ya Baiolojia, Kemia , Kilimo na Fizikia kwa shule nne za sekondari ikiwa ni sehemu ya hatua za kukabili changamoto za matokeo mabaya ya shule za sekondari za wilaya hiyo Hususan katika masomo ya sayansi.
Mkuu huyo wa Wilaya mbali na kuwashukuru walimu hao kwa kufika wilayani humo.

Pia alitoa wito kwa Jamii kujenga Nyumba Bora hususan Vijijini ili kusaidia watumishi wanaopangwa huko kwa huduma za jamii zikiwemo Elimu na Afya kutokana na mazingira ya kusomea kutokuwa yenye mvuto ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa zana muhimu na maabara, na kwamba hatua ya kusambazwa kwa teknolojia hiyo rahisi licha ya kuwawezesha wanafunzi sasa kujifunza katika hali iliyobora zaidi kwa vitendo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Bw Addo Mapunda aliwasihi walimu hao kufanya kazi kwa kuwa Wilaya hiyo inaupungufu mkubwa wa walimu hususan vijijini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw Ally Mohamed Mtopa alitoa ahadi ya kununua kitanda na godoro kwa walimu watakaopangwa katika kata yake lakini pia aliwageukia walimu hao kuhusiana na suala la migomo ya walimu ambapo aliwasihi kutojiingiza katika masuala hayo badala yake aliwaomba walimu hao kufikisha malalamiko yao kwa Madiwani ambao ndio wenye maamuzi ya Halmashauri hiyo
Baadhi ya walimu hao.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye tukio hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega akitoa nasaha zake kwa walimu hao
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa akiwakaribisha walimu wapya

No comments:

Post a Comment