Pages

Pages

Thursday, March 07, 2013

Mwanamuziki mkongwe afariki Dunia


































Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MMWANAMUZIKI wa siku nyingi nchini, Kabeya Badu, pichani, amefariki Dunia, wakati maisha yake ya muziki aliyamalizia katika bendi ya Wazee Sugu, huku akifia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam, apokuwa amelazwa kwa kwa matibabu ya figo.

Taarifa za msiba wa mwanamuziki huyo mkongwe zimethibitishwa katika ukurasa wa facebook ya mkongwe mwingine, John Kitime, ikielezea mshtuko wa kifo hicho.

Enzi za uhai wake, kabla ya Wazee Sugu, Badu alipigia bendi bendi mbalimbali zikiwemo Orchestra Fovette, Orchestra Safari Sound, Orchestra Marquis, Intimate Rhumba, Tancut Almasi na nyinginezo.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu.

No comments:

Post a Comment