Pages

Pages

Friday, March 08, 2013

Uhuru Kenyatta aendelea kutesa kileleni uhesabuji kura Kenya



Uhuru Kenyatta

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MATOKEO ya kimbunga cha uhesabu kura nchini hapa yanaendelea, huku mgombea Uhuru Kenyatta akiongoza kwa kura 4,769, 769, wakati mpinzani wake 4,132, 062, hivyo Kenyatta akiwa zaidi ya kura 637 7 07.

Matokeo hayo ni kuashiria kuwa Kenya wamedhamiria kufanya maajabu, kama hali hiyo itaendelea, ingawa upande wa Odinga wametishia kugomea matokeo ya uhesabuji huo wa kura.

Uchaguzi nchini hapa ulianza tangu Jumatatu kwa kujionea Wakenya wengi wakihudhuria katika vituo vya upigaji kura kwa ajili ya kutimiza haki zao za msingi kwa kuwachagua viongozi wao.

Mara baada ya kuhesabu kura kuanza, Tume ya Uchaguzi ilitangaza kusitisha kuhesabu kwa kutumia mtambo kwa madai kuwa ulikuwa na hitilafu, hivyo kuanza kuhesabu kwa mkono.

No comments:

Post a Comment