Pages

Pages

Thursday, March 07, 2013

Uchaguzi Mkuu Kenya: Upande wa Odinga wataka uhesabuji kura usitishwe, huku akiwa nyuma kwa kura 664198



Na Mwandishi Wetu, Kenya
WAKATI matokeo yakiendelea kupatikana kwa Uhuru Kenyatta kuongoza kwa kura 2,660,379, akifuatiwa na Raila Odinga, aliyepata kura 1,996,181,  upande wa Odinga umetaka shughuli za uhesabuji wa kura kusitishwa katika Ukumbi wa Bomas.

Uhuru Kenyatta angali anaongoza kwa idadi ya kura za wagombea wa urais akiwa na kura 2,660,379 dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga aliye na kura 1,996,181 lakini matokeo rasmi yatajulikana tu mwishoni mwa juma.

Habari hizo zimeubua hisia na wasiwasi katika Uchaguzi huo nchini hapa, ikiwa ni matokeo magumu yanayoweza kuleta mtafaruku miongoni mwa Wakenya.

Hatua hii imelazimu tume hiyo kuanza kuhesabu kura upya katika kitovu cha kupokea matokeo ya kura za urais kwenye ukumbi wa Bomas viungani wa mji wa Nairobi.

Kalonzo Musyoka ambaye ni mgombea mwenza wa Raila Odinga, amehutubia waandishi wa habari mjini Nairobi na kusema kuwa muungano wa CORD, unataka shughuli hiyo ya kuhesabu kura za urais kusitishwa mara moja na kuanzishwa upya wakitumia stakabadhi kutoka kwa makarani wa kura jambao ambalo linafanywa kwa sasa

Aliendelea kwa kusema kuwa baadhi ya matokeo yako juu kuliko idadi ya wapiga kura katika baadhi ya maeneo ambako kura zilipigwa, huku akisema kuwa tatizo hilo limetokana na kugoma kwa mitambo ya kupiga kura.

No comments:

Post a Comment