Pages

Pages

Monday, March 04, 2013

Uchaguzi Mkuu Kenya, kundi lavamia na kuua watu 12




Na Mwandishi Wetu, Kenya
Watu 12 wamekufa leo Kilifi, Mombasa nchini Kenya, ikiwa ni siku ambayo Taifa hilo lipo kwenye Uchaguzi Mkuu wa kumtafuta Rais, huku wagombea wenye majina wakitikisa, akiwamo Raila Odinga, Uhuru Kenyatta na wengineo.

Vifo hivyo vimetokana na kundi la watu kuvamia polisi waliokuwa doria na kufanya unyama huo katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu.
 
Hata hivyo, chanzo cha vifo hivyo haijajulikana, ingawa kumekuwa na rabsha za hapa na pale katika Uchaguzi huo, ikiwamo watu wanaolalamika kutokuona majina yao katika Tume ya Uchaguzi, ingawa baadaye waliambiwa kuwa hakuna mtu aliyejiandikisha halafu akashindwa kupiga kura.

Mdau wa Handeni Kwetu aliyepo nchini Kenya, alisema kuwa kwa ujumla hali ni nzuri katika Uchaguzi huo, katika siku ambayo Taifa hilo linapiga kura.

Mdau huyo alisema licha ya watu kulalamika majina yao kuwa hayaonekani, lakini watu wengi hawakujitokeza mapema kuangalia majina yao walipotakiwa kufanya hivyo na Tume ya Uchaguzi nchini hapa.

Habari zaidi za Uchaguzi huo zitaendelea kutolewa katika blog yako hii, kwa ushirikiano mkubwa na wadau waliokuwapo nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment