Pages

Pages

Wednesday, March 06, 2013

TASWA watoa tamko kujeruhiwa Absalom Kibanda



Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili alipolazwa kwa matibabu.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA),inaungana na waandishi wa habari wote kulaani kitendo cha watu wasiojulikana kumvamia na kumjeruhi vibaya mwenyekit wa Jukwaa la wahariri, Absalom Kibanda.


Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto, alisema kuwa watu hao waliohusika wakamatwe ili sheria ichukue mkondo wake.
Tusingependa Kama waandishi kuamini yanayosemwa lakini kutokana na uadilifu mkubwa wa vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama kuwapata watu ambao wamehusika na tukio hilo.

Sisi tunaamini tukio hili la mwenzetu kuvamiwa na watu hao halikuwa kwa bahati mbaya ni Jambo ambalo linaonekana Kama limepangwa na Kama ni hivyo lengo na madhumuni yake ni nini kwa waandishi wa Tanzania? Uhuru na Usalama wa waandishi upo wapi?

Katakana na tukio hili la mpiganaji na Kiongozi wetu kuvamiwa ,ipo haja ya sisi waandishi kuungana pamoja katika kutafuta Usalama wetu.kuna matukio mengi ya waandishi yametokea na tumekuwa tukipiga kelele lakini matokeo yake hakuna hatua ambazo serikali inayafanyia kazi.

Katakana na majeraha maki wa aliyopata mwenzetu,tunaiomba serikali na hats Mheshimiwa Rais,Dr Jakaya Kikwete kutoa Masada wa mwenzetu kwenda kutibiwa nje,tunaamini serikali ni sikivu na Rais wetu ni mwenyeji kusikia kilio cha watu wake.

Kibanda na wenzak ndani ya Jukwaa la wahariri wamekuwa mstari wa mbele katika kurudisha hadhi ya tasnia ya habari na kujenga umoja miongoni mwa waandishi wa habari na kuifanya tasnia ya habari kuheshimika tofouti na ilivyokiwa nyuma.

Tunaungana na kampuni ya habari, wafanayakazi wenzak, familia yake na waandishi wote kwa jumla na kumuomba mungu ampomye ili tuweze kuunganae nae katika kusaidia kupasha habari Watanzania lakini ili aweze kuwaongoza waandishi wenzake

No comments:

Post a Comment