Pages

Pages

Tuesday, March 05, 2013

Masikini Odinga, Kenyatta aendelea kuchanja mbuga Urais Kenya



Uhuru Kenyatta, mgombea urais Kenya.

Na Mwandishi Wetu, Kenya
MGOMBEA Urais nchini Kenya, Uhuru Kenyatta, ameendelea kukalia kileleni katika matokeo yanayoendelea kutolewa nchini hapa kwa kupata kura 2,590,393.


Matokeo hayo yalitangazwa saa 14:40, huku Raila Odinga, yeye akifuata kwa kujinyakulia kura 2,001,651, wakati Musalia Mudavadi na yeye akipata kura 136,351.

Hayo ni matokeo yanayoashiria kuwa mwelekeo wa Uchaguzi huo bado upepo upo kwa Kenyatta, anayechuana na mtu ambaye mwaka 2007 alikuwa juu mno akipendwa na Wakenya wengi na kusababisha kuundwa kwa serikali ya mseto kati yake na Mwai Kibaki.

Kura hizo zinahesabiwa kutoka vituo zaidi ya 33 huku mpaka sasa kura hizo zikihesabiwa kutoka zaidi ya nusu ya vituo vilivyoteuliwa kupigiwa kura katika Taifa la Kenya mwaka huu.

Mungu ibariki Kenya na uendelee kuwa Uchaguzi wa amani.

No comments:

Post a Comment