Pages

Pages

Wednesday, March 06, 2013

Mmama amwaga machozi kwa kuminywa na gari



Daladala ikionekana jinsi ilivyoharibika sehemu za kuingilia, ambapo abiria huyo alibanwa kwenye uwazi huo unaoonekana.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MAMA ambaye hajajulikana jina lake mara moja, alijikuta akiianza siku vibaya baada ya kubanwa na gari katika mminyano wa kugombania gari za kutoka Kimara kuelekea Posta.
Daladala hiyo ikionekana kwa nyuma

Tukio hilo lilitokea mapema leo katika kituo cha Daladala cha Kimara Mwisho, ambapo kuanzia asubuhi kunakuwa na mvutano mkali wa kugombania magari ili kila mmoja awahi kwenye sehemu yake ya kazi.

Mara baada ya daladala hiyo yenye namba T 765 AXL kusimama kwenye kituo hicho, watu walianza kugombania gari hilo, hata hivyo sekunde moja hadi kumi, kilio kikali cha kwikwi kilianza kutokea na kushtua wengi.

"Mama yangu wee.. Mguu wangu, nimebanwa jamani naombeni msaada wenu. Ohhhaa mama wewe".. Hizi zilikuwa sauti kutoka kwa mama huyo, ambaye wakati huo jasho jembamba lilikuwa likimtoka akilia mguu wake.

Gari hilo sehemu za kukanyagia kwenye mlango wake uliharibika, hivyo kuwa na uwazi, jambo ambalo lilisababisha mguu wa mama huyo kuingia hapo na kubanwa, hasa pale watu walivyokuwa wanazidi kugombania kuingia kwenye usafiri huo.

Katika hali ya kushangaza, licha ya mama huyo kuzidi kulia kwa dakika zaidi ya 10, lakini wengi wao walimpuuza wakiingia ndani ya daladala kuwahi siti za kuwafikisha kwenye sehemu zao za kazi, jambo lililoshangaza umma.

No comments:

Post a Comment