Pages

Pages

Monday, March 25, 2013

Taifa Stars, Morocco waingiza Milioni 226


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah
Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia  kati ya Tanzania (Taifa Stars) na
Morocco (Lions of the Atlas) iliyochezwa jana (Machi 24 mwaka huu) na
Stars kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 226,546,000.



Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 32,614 waliokata tiketi
kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh.
10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 34,557,864.41, maandalizi ya mchezo
sh. 28,450,000 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh.
8,625,641.88.

Nyingine ni bonasi kwa timu ya Taifa Stars sh. 28,798,220.34, asilimia
15 ya uwanja sh. 18,917,141.01, asilimia 20 ya gharama za mechi sh.
25,222,854.67 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF) sh. 6,305,713.67.

Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh.
71,885,135.82 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,783,428.20 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.

No comments:

Post a Comment