Pages

Pages

Saturday, March 23, 2013

Sanaa usipokuwa makini, utamegwa na kila mtu



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Msanii anayetamba na kibao chake cha Baba Awena kutoka taasisi ya kulea Vipaji ya Tanzania House of Talents (THT), Pili Juma, maarufu kama Vida, amesema kuwa kwenye sanaa mtu asipokuwa makini atafanya mapenzi na kila mtu kutokana na vishawishi wanavyokutana navyo.
Mkali wa kibao cha 'Baba Awena', Vida kutoka (THT), akifunguka kuwa sanaa usipokuwa makini utamegwa na kila mtu.

Akizungumza na Handeni Kwetu, Vida alisema jambo hilo linasababisha msuguano na cheni ya ngono, huku akisema umakini unatakiwa ili wasanii hao ‘wasimegwe’ kutokana na waoa kujiingiza kwenye sanaa.

"Sanaa sio uhuni, ila ukiwa hujitambui utamegwa na kila mtu, hivyo lazima kila msanii ajitambuwe na kuwa na mkazo na lile jambo analohitaji katika maisha yake, maana kama ni umalaya sekta zote hayo yapo.

"Naamini wasanii wakijitambua, suala hilo halitakuwapo na kama likiendelea kuwapo, basi ni tabia ya mtu na wala hajachochewa na matokeo ya kuingia kwenye sanaa, japo nakubali kuwa vishawishi ni vingi,” alisema Vida.

Vida ni miongoni mwa wasanii wa kike mwenye muonekano mzuri pamoja na kubebwa na mvuto wa sauti yake katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva.

No comments:

Post a Comment