Pages

Pages

Sunday, March 24, 2013

Ridhiwani Kikwete ainanga klabu ya Simba


Ridhiwani Kikwete

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Kamati ya Jengo la Mafia la Klabu ya Yanga, Ridhiwani Kikwete, amesema kwamba wataiabisha Simba kwa kuhakikisha kuwa wanaiweka klabu yao katika nembo ya kibiashara na mafanikio lukuki.

Ridhiwani aliyasema hayo mapema wiki hii, mara baada ya kuteuliwa na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo sambamba na kumpa mamlaka ya kuteua watu anaotaka kufanya nao kazi kwenye kamati hiyo.


Akizungumza mapema wiki hii, Ridhiwani alisema kwamba hawaitaji kupiga soga katika mambo ya kimaendeleo, hivyo wadau wa Simba wajiangalie mara mbili.

Alisema lengo kubwa ni kuhakikisha kuwa kila mtu anafanya mambo yenye maendeleo na Yanga, hivyo wenye mapenzi mema na klabu yao ni wakati wa kushirikiana na kusubiri mafanikio yao.

“Wale ndugu zetu wa upande wa pili, Simba SC wajiandaye pia kusubiria mafanikio kutoka kwetu, maana tutafanya kazi kwa moyo na mapinduzi makubwa nchini.

“Huu ni wakati kuiweka Yanga kwenye kilele cha mafanikio na sio kupiga porojo, hivyo naamini mambo yatakuwa mazuri na hakika watu wataishia kuchungulia mafanikio kutoka kwetu,” alisema.

Kamati ya Ridhiwani itahusika na kupitia na kuratibu ujenzi wa jingo la Mafia, Kariakoo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhakikisha kuwa klabu yao inajiendesha kibiashara.

No comments:

Post a Comment