Pages

Pages

Saturday, March 23, 2013

Usiruhusu tamaa ya kutembea na swahiba wa mpenzi wako


MAMBO FULANI MUHIMU
Usingizi wa dhahabu
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KUNA vitu ambavyo vinashangaza, vikiwamo hivi vya mtu kujiachia, kuendekeza tamaa kiasi cha kutoka kimapenzi na mtu ambaye ana urafiki wa karibu na mke au mpenzi wake.

Tabia hii haifahai katika jamii. Kwa bahati mbaya inafanywa na watu ambao wana pepo la ngono. Ukiwaona kwenye maeneo yao, wakiwa na hao wasichana au wavulana, hujifanya wenye tabia nzuri, kumbe ni mafedhuli katika uhusiano wa kimapenzi.


Hili si jambo la busara. Kila mtu anapaswa kujiangalia, namna gani anaweza kuilinda heshima yake kwa mpenzi  au mke wake, kiasi cha kujichunguza na kuzuia matamanio yake kwa wanaopita mbele ya macho yake, wakiwamo marafiki wa watu wao.

Kwa mfano, mtu anaweza kumpenda kweli mke au mpenzi wake kiasi cha kuwa karibu kila mahali. Watu hao hukesha wakifurahia uhusiano wao, wakiona hakuna mwingine wa kuzuia pendo lao.

Lakini, katika safari ya uhusiano wao, mmoja wao anaweza kubadilika ghafla anapofanikiwa kukutana au kuonana na rafiki wa mpenzi wake, hivyo kuonyesha tofauti kubwa.

Utamuona ananza kujishusha au kujionyesha kwa kila jambo. Hufika mbali zaidi na kulazimisha kutoka naye ‘out’. Na wale wanaojifanya wanaishi Dunia ya Dijitali, hubaki kimya na kuona marafiki zao wana haki ya kwenda popote, hata kwenye majumba ya starehe.

Wataalamu wa mambo ya vinywaji vikali, wanasema zipo pombe au vinywaji ambavyo vinaleta msukumo mkubwa katika tendo la mapenzi. 

Mara baada ya kupiga chupa mbili au tatu, vinywaji hivyo huwalainisha zaidi watoto wa kike na kujikuta wakitamani kufanya mapenzi wakati wowote kutoka hapo alipo.

Nisingependa kukitaja hicho kinywaji kwa sababu za kimaadili, ingawa ukweli utabaki hivyo hivyo. Ukiangalia hapo, kama rafiki huyo ametoka na mpenzi wako na ameshikwa na hamu ya kufanya tendo la ngono, nini afanye ili kujiondolea hamu yake?

Ikumbukwe kuwa, rafiki huyo ametoka na mpenzi wako na upo uwezekano kuwa mpenzi wake yupo mbali. Hivyo kuachana na mtu wako bila kuondolewa hamu yake ni jambo gumu.

Tena kama mtu wako, hasa mwanaume akiwa mwepesi, mlaini na mwenye tama ya watoto wa kike, hakika lazima atakuwa ameingia kwenye ulimwengu wa mapenzi na rafiki yako.

Katika suala kama hilo, kuna mambo mengi husababisha hayo, lakini mwisho wa siku ukweli utabaki kuwa ni upungufu wa maadili, tabia mbaya ya kuona yoyote unaweza kulala naye kitanda kimoja na kucheza kwenye Dunia ya mahaba.

Mbaya zaidi, Dunia hiyo ya mahaba unataka kufanya na kila mtu, wakiwamo marafiki wa wapenzi wenu ambao kwa hakika hapo kabla mlikuwa mnaheshimiana kupita kiasi.

Je, wewe ni miongoni mwa waathirika ambao wapenzi wao, wake zao, wachumba zao wametoka kimapenzi na marafiki zao? Je, mtu wako alianzaje hadi kugundua kuwa anatoka na rafiki yako?

Ingawa zipo sababu lukuki ambazo hapa hazitaweza kumalizika kwa mara moja, hivyo nitaendelea kuelezea hatua kwa hatua kila nipatapo muda na pumzi kwa ajili ya kupeana ushauri katika mambo ya mapenzi.

Nakushukuru kama wewe ni msomaji mkubwa wa safu hii, huku nikiahidi kuwa karibu na wewe kupeana ujuzi wa aina yoyote. Kwa wewe ambaye unapenda zaidi kusoma mitindo na athari zake, ni vyema ukaomba msaada kwa kupitia mawasiliano yangu hapo chini.

Zipo mbinu nyingi na ujuzi wa kuweza kumudu mambo ya mapenzi kwa namna moja ama nyingine na ukumbi mpana wa kujulishana hili na lile kwa kuhakikisha kuwa unaendelea kuwa msomaji wa safu hii. 
0712 053949
0753 806087

No comments:

Post a Comment