Pages

Pages

Sunday, March 24, 2013

Mashindano ya Gambo Cup Korogwe yamwagiwa sifa



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Chama Cha Soka wilayani Korogwe, Peter Juma, amesema licha ya kuwa na changamoto za hapa na pale, lakini ligi yao iliyoanzishwa na Mkuu wa Wikaya, Mrisho Gambo inaendelea vizuri kwa vijana kuonyesha vipaji vyao.
Mrisho Gambo, Mkuu wa wilaya Korogwe
Akizungumza kwa njia ya simu, Juma alisema kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika ligi hiyo, ikiwamo uwezo wa uchezaji wa vijana wao.


Alisema ligi hiyo yenye vituo nane wilayani humo, pia ina ushindani wa aina yake, hivyo wanaamini kuwa lengo haswa la kuwaweka vijana pamoja na kujadili suala la michezo limefanikiwa.

“Namshukuru DC kwa kuanzisha ligi ya Gambo Cup wilayani Korogwe, maana tunajua kuwa ni njia nzuri ya kutupatia mafanikio katika suala zima la mpira wa miguu.

“Timu nyingi zimejitokeza na zinashiriki kwa kasi ya ajabu, hivyo tunaamini kuwa ni njia moja wapo ya kutangaza vipaji vya wachezaji wetu kwa kupitia mashindano ya Gambo Cup,” alisema.

Vituo ambavyo vinashiriki mashindano hayo ya Gambo Cup wilayani Korogwe ni pamoja na Bungu, Kelenge, Old Korogwe, Kwamndolwa, Kwamsisi, Makuyuni, Mswaha, Mombo na New Korogwe, iliyopo Korogwe mjini.

No comments:

Post a Comment