Pages

Pages

Thursday, March 14, 2013

Serikali yanywea urushwaji matangazo wa Digitali



Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Makame Mbalawa, amesema kuwa watazungumza na wadau wa habari, wanaomiliki vituo vya televisheni kuweza kuangalia malalamiko yao.

Mapema wiki hii, wamiliki wa vituo vya televisheni, wakiongozwa na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, inayomiliki wa ITV walisema kuwa kuna haja ya serikali kurudisha matumizi ya urushwaji wa matangazo kwa njia ya analogy badala ya digital, kama ilivyokuwa sasa.

Akizungumzia mchakato huo kwenye kituo cha Radio One, Mbalawa, alisema kuwa hakuna kitu kisichowezekana, hivyo anaamini watakaa na kuangalia maombi yao.

Licha ya serikali kuwataka wananchi watumie ving’amuzi, lakini imebainika kuwa urushwaji huo una matatizo mengi, hivyo kuwakosesha uhuru wa habari wananchi wao.

No comments:

Post a Comment