Pages

Pages

Sunday, March 31, 2013

Tunawatakia Pasaka Njema, ila Amani itawale


LEO Jumapili, Wakristo wote Tanzania wanaungana wenzao duniani kote kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka, ikiwa ni kufufuka kwa Yesu Kristo.

Siku ya leo ni muhimu kwa Wakristo wote, huku ikianzia tangu juzi Ijumaa Kuu, hivyo ni wakati wa waumini wote na wale wasiokuwa waumini wa dini hiyo kuadhimisha kwa Amani na upendo.
Mara kadhaa, wapo baadhi ya watu ambao hutumia siku za Sikukuu

Hofu yatanda ghorofa lililoanguka na kupoteza uhai wa watu 21



NaMwandishi Wetu, Dar es Salaam
LICHA ya kufikia idadi ya watu 21 hadi sasa ambao wameshapoteza maisha katika tukio la kuanguka kwa ghorofa mitaa ya Indira Ghandi juzi jijini Dar es Salaam, inatarajiwa kuongezeka kwa marehemu kutokana na mwingiliano wa watu katika eneo hilo.

Watu hao waliofariki wengineo wamekatwa mikono, miguu, vichwa na kupata majeraha makubwa mwilini.
 
Baadhi ya watu waliokuwapo kwenye tukio hilo, wanasema kuwa idadi hiyo ni ndogo kulinganisha na pilika pilika za watu waliokuwapo kwenye eneo hilo, kama Mama Lishe, Ombaomba na wengineo.

Aidha, pembeni yake kulikuwa na msikiti na madrasa ndani yake ambapo watu hao wanaosadikiwa kufunikwa na kifusi bado hawajapatikana mpaka sasa.

Vida aachia video ya Baba Awena, full utamu


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI anayeibukia kwa kasi katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya anayetokea katika taasisi ya kukuza na kulea vipaji ya Tanzania House of Talents (THT), Pili Juma, maarufu kama Vida, ameachia video yake ya 'Baba Awena' ikiwa na full utamu.
                     Vida akionyesha poziiii
Video hiyo iliyokuwa kwenye kiwango cha juu ameitengeneza chini ya ufundi wa John Kallage, huku akimshirikisha mkali mwingine wa muziki huo, Linex ambaye naye anatokea THT.

Green Stone kuwafuata Mgambo Shooting Tanga


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TAWI la Yanga la Green Stone, limetangaza kuwafungia safari timu ya Mgambo Shooting, Aprili 13 mwaka huu kwa ajili ya kwenda kutangaza ubingwa na timu yao wakiwa na shangwe za kila aina.
Yusuphed akikabidhi kadi ya uanachama wa Yanga, hivi karibuni kwa kupitia tawi lao la Green Stone.
Safari hiyo itakuwa ya kwanza kwa tawi hilo kuambatana na timu yao baada ya kuanzishwa mapema mwaka huu na kutambuliwa na klabu ya Yanga, hasa baada ya

Saturday, March 30, 2013

Edward Lowassa mgeni rasmi Sokoine Marathon Arusha

Na Mwandishi Wetu, Arusha
WAZIRI Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika mbio za Sokoine Marathon, zinatakazofanyika, Aprili 12, mwaka  huu, wilayani Monduli, mkoani Arusha.





Lowassa


Mbio hizo zitafanyika katika kijiji alichozaliwa na kuzikwa waziri mkuu Edward Moringe Sokoine ikiwa ni siku ambayo taifa itaadhimisha kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo mkuu katika historia ya taifa la Tanzania.

Akithibitisha hilo Mratibu wa mbio za Sokoine Marathon 2013, Wilhelm Gidabuday alisema kuwa tayari wameshapata uthibitisha wa kuwepo kwa kiongozi huyo akiongozana na viongozi wengine wakuu wa nchi wakiwemo Mawaziri na Wabunge.

“Kutokana na wadhifa na heshima aliyokuwa nayo Marehemu Sokoine tumeona ni vizuri kuwaalika viongozi wetu wakuu wa nchi,n watu wengi tu watakuwepo, wabunge, mawaziri wakiongozwa na mheshimiwa Lowassa, wananchi wa kada  mbalimbali, lengo ni kumpa heshima inayostahili kingozi wetu,” alisema Gidabuday.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya maandalizi aliyepewa jukumu la kuwasiliana na viongozi ikiwa ni pamoja na Mgeni Rasmi, Mbunge wa viti maalum jimbo la monduli (CCM), Namelok Sokoine alisema kuwa, tayari wameshapata uhakika wa uwepo wa Lowassa katika mbio hizo.


Sokoine

likuwa tunatarajia kumpata kiongozi wetu wa nchi Mbio za Sokoine Marathon ambazo ni za kwanza kufanyika katika historia ya nchi hii katika maadhimisho ya kumbkumbu ya kifo cha kiongozi wa ngazi za juu wa taifa letu zinatarajiwa kushirikisha wakimbiaji zaidi ya 500 ambapo mpaka sasa tayari wanariadha 300 wameshathibitisha kushiriki.

Akizungumzia swala la kutoa namba pamoja na usajili, Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Arusha (ARAA), Joseph Jorwa alisema tayari utaratibu wa kuandaa namba umeshakamilika na kuongeza kuwa zoezi la usajili utafanyika baada ya sikuukuuu za Pasaka, katika Ofisi za ARAA, zilizoko katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwa ada ya sh. 2000 za Tanzania.

Sokoine Marathon zitahusisha mbio za kilometa 10 na kilometa 2 kutembea na kukimbia na zitatanguliwa na misa maalum zitakazofanyika katika kanisa la katoliki alililokuwa ni muumini kijijini kwake na zinatarajia kukutanisha watu mbalimbali kumuombea kiongzi huyo.

Unaijua Yanga au unaisikia, leo balaa Morogoro

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TIMU ya Polisi Morogoro, leo itakuwa na kibarua kigumu mbele ya vinara wa ligi ya Tanzania Bara, Yanga SC, pale zitakapovaana katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, katika mfululizo wa mechi za Ligi hiyo inayodhaminiwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania.
 Wachezaji wa Yanga wakijifua
Yanga inaingia uwanjani huku ikiwa kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Bara kwa kujikusanyia jumla ya pointi 48, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 40, wakati Simba yenyewe ina pointi 34.

Idadi ya vifo yaongezeka ghorofa lililoanguka jana



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HALI ya uokoaji katika jengo la ghorofa 16 lililoanguka jana mtaa wa Indira ghandi, Kariakoo jijini Dar es Salaam inaendelea, huku hadi sasa watu 18 wakiwa wamekutwa wameshapoteza maisha.
Pichani, uokoaji ikiendelea
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Saidik, alitembelea muda sio mrefu kwa ajili ya kujionea hali ya uokoaji inavyoendelea katika eneo hilo lililoibua taharuki kubwa.

Jana, Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, alitembelea pia katika eneo hilo na kujionea jinsi lilivyoanguka na kusababisha mtafaruku mkubwa kwa watu waliokuwa kwenye kadhia hiyo.

Juhudi za kuokoa watu waliokuwa kwenye ajali hiyo zilipamba moto dakika chache baada ya habari hizo kufika kwa vyombo vya Dola, huku viongozi wa vyama vya siasa na serikali kuwa bega kwa bega katika kufanikisha juhudi za kunusuru roho za watu wao.

Mwili mmoja umeopolewa muda mfupi uliopita, ikiwa ni masaa kadhaa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Sadik kufika, wakati tayari idadi ya watu 17 ilishatangazwa tangu jana.