Pages

Pages

Sunday, March 31, 2013

Green Stone kuwafuata Mgambo Shooting Tanga


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TAWI la Yanga la Green Stone, limetangaza kuwafungia safari timu ya Mgambo Shooting, Aprili 13 mwaka huu kwa ajili ya kwenda kutangaza ubingwa na timu yao wakiwa na shangwe za kila aina.
Yusuphed akikabidhi kadi ya uanachama wa Yanga, hivi karibuni kwa kupitia tawi lao la Green Stone.
Safari hiyo itakuwa ya kwanza kwa tawi hilo kuambatana na timu yao baada ya kuanzishwa mapema mwaka huu na kutambuliwa na klabu ya Yanga, hasa baada ya
kugawa kadi kwa wanachama wao.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, mlezi wa Green Stone, Yusuph Shaban Mhandeni, alisema kwamba wanaamini wanachama wote waliokuwa kwenye tawi lao watapata nafasi ya kuhudhuria kwenye mchezo huo wa Yanga na Mgambo, ambapo wao watatangaza ubingwa.

Alisema kwa sasa wanaombea mema timu yao ifanye vyema katika michezo yake miwili, ukiwamo wa Yanga na Polisi Morogoro pamoja na Ruvu Shooting, ambapo kwa pamoja zitatoa nafasi ya ubingwa kwa timu yao.

"Tumejiandaa kufanya makubwa tukiwa ndani ya klabu yetu ya Yanga, hivyo naamini tutakuwa pamoja katika mechi ya Mgambo Shooting ambapo tutatangaza ubingwa wetu.

"Itakuwa mara ya kwanza kwenda kwenye mechi za Yanga kama tawi rasmi la Yanga, hivyo nadhani matawi mengine yatajua namna gani tumedhamiria kuwa wanachama wenye tija na Yanga,” alisema Mhandeni.

Tawi la Green Stone lenye maskani yake Mwananyama Mwinjuma, jijini Dar es Salaam, lipo chini ya Lumolwe Matovolwa, maarufu kama Big, ambaye pia ni msanii nguli wa filamu hapa nchini.

No comments:

Post a Comment