Pages

Pages

Sunday, March 31, 2013

Vida aachia video ya Baba Awena, full utamu


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI anayeibukia kwa kasi katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya anayetokea katika taasisi ya kukuza na kulea vipaji ya Tanzania House of Talents (THT), Pili Juma, maarufu kama Vida, ameachia video yake ya 'Baba Awena' ikiwa na full utamu.
                     Vida akionyesha poziiii
Video hiyo iliyokuwa kwenye kiwango cha juu ameitengeneza chini ya ufundi wa John Kallage, huku akimshirikisha mkali mwingine wa muziki huo, Linex ambaye naye anatokea THT.


Akizungumza jijini Dar es Salaam Vida alisema video ya wimbo huo ameitambulisha kwa ajili ya kuwapatia burudani zaidi mashabiki wake baada ya kuachia wimbo huo hivi karibuni.

Alisema wadau wengi watapata kuona kipaji chake alichoonyesha katika wimbo huo akifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na mwimbaji mwenye uwezo wa kutisha, Linex.

“Nashukuru nimefanikiwa kukamilisha video ya wimbo wangu wa Baba Awena uliotengenezwa na John Kallage, huku nikiamini kuwa upo kwenye kiwango cha juu mno na utakosha watu wengi.

“Nimefanya kazi ya maana kwa ajili ya kuonyesha uwezo wangu, hivyo naamini wadau na mashabiki wataendelea kuipokea video ya wimbo huo wa Baba Awena inayonitambulisha rasmi katika sanaa,” alisema Vida.

Vida ni miongoni mwa wasanii wanaotokea katika taasisi hiyo ya THT inayozalisha wasanii mahiri chini ya Ruge Mutahaba, huku baadhi ya wakali walioibukia hapo akiwa ni Barnabas, Amini, Linah, Mwasiti na wengineo wengi.


No comments:

Post a Comment