Pages

Pages

Monday, February 04, 2013

TPBC yawarushia kombora mabondia wake



Rais wa TPBC, Onesmo Ngowi

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini TPBC inewataka mabingwa wake wote wawe wametetea mikanda yao ya ubingwa ifikapo tarehe 30 Marchi kwaka huu ili kuepuka kunyanganywa.

Kwa kipindi kirefu mabingwa kadhaa wamekuwa wanakaa na mikanda bila kuitetea. Tunataka ieleweke kuwa muda wa kukaa na ubingwa wa TPBC ni miezi sita (6) tu na sio mwaka mmoja.

Taarifa iliyotumwa na Imetolewa na Onesmo Ngowi, Rais TPBC ilisema kuwa bingwa wa kweli anatakiwa awe anafuata sheria, kanuni na taraibu za ubingwa alionao na sio kujiita bingwa wakati hufuati masharti yaliyowekwa.

Katika kipindi hiki cha mwaka 2013 tunawataka mabondia waheshimu sheria za mikataba wanayotiliana sahihi na mapromota. Tunataka ngumi ziboreshwe kakini pamoja na changamoto nyingi zilizoko, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wadhamini, mabondia wakiheshimu mikataba yao mchezo wa ngumi utakua na kuwavutia wadhamini.

Tunapenda pia kuwaomba wenye mapenzi mema na nchi hii wajitolekeze kwa wingi ili kushirikiana na sisi tuiweke Tanzania kwenye chati ya dunia kama zilivyo nchi nyingine.


No comments:

Post a Comment