Pages

Pages

Monday, February 04, 2013

Maofisa Ardhi Manyoni wasimamishwa kazi

 

Mkuu wa Mkoa Singida, Dk. Perseko Vicent Kone

Na Salesi Malula, Manyoni
SAKATA la Migogoro ya Ardhi ambayo imedumu kwa muda mrefu Wilayani Manyoni kutokana na Shinikizo la Wananchi kuwaondoa Maafisa Ardhi, limefanikiwa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Perseko Vicent Kone kuwasimamisha kazi kwa muda usiojulikana.

Katika  Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mnadani eneo la Majengo wilayani Manyoni ambapo Mkuu wa Mkoa wa Singida alikuwa katika ziara yake ya kikazi aliwaruhusu wananchi 45 kutoa kero mbalimbali ambazo zinawakabili.


Mkuu wa Wilaya Manyoni Bi.Fatma Hassan Toufiq aliwatembelea wananchi wa eneo la Majengo na Kipondoda na kuombwa kuwatimua Afisa Ardhi Leonard Msafiri, kwakuwa amekuwa kero kubwa katika wilaya ambapo alikuwa akipora viwanja vya wananchi pasipo kufuata taratibu wala kuwalipa fidia wananchi wanaomiliki maeneo yao.

Mkuu wa Mkoa wa Singida katika ziara yake ya siku tatu wilayani Manyoni akiwa katika eneo la Majengo na kipondoda aliweza kukutana na madudu ambayo yalikuwa yakifanywa na Maafisa hao wa ardhi.

Wananchi 45 waliweza kutoa kero zao kuhususiana na kuporwa meneneo yao bila kulipwa fidia na maafisa wa ardhi ambao walikuwa wakitajwa kwa majina huku baadhi ya watoa kero wakilia kwa uchungu na kumuomba RC kuingilia kati sakata hilo.

Akijibu kero zao katika mkutano wa Hadhara DK.Kone alisema amesikia kilio cha wananchi wa Manyoni na kuanzia sasa 

“Ninasimamisha Shughuli zote za ugawaji na upimaji wa Viwanja wilayani Manyoni mpaka pale maeneo yote yanayolalamikiwa yawe yamepatiwa ufumbuzi, na nimesimamisha shughuli zote za ujenzi kwenye maeneo yote yanayolalamimikiwa na kuanzia sasa nawasimamisha kazi maafisa, Ardhi wanaolalamikiwa Leonard Msafili, John Chima na Kenedi Chigulu ambao wamesababisha malalamiko haya”.

Huku akishangiliwa na wananchi alisema “Naunda Tume ya wataalamu watakaotoka Mkoani, ni tume itakaoshirikisha wataalamu mbalimbali watakaochunguza mgogoro wote na wanipe mapendekezo, Tume hiyo inatarajia kuanza kazi Februari 4, huku ikifanya kazi kwa muda wa siku saba kwa kuwahoji wote.

"Nataka kupitia mgogoro huu wa masuala ya Ardhi kwakuwa ni fundisho kwa watumishi wote ambao siyo waadilifu na wanaotakiwa wafukuzwe au kupewa onyo.

Aidha wengine wataburuzwa kortini bila kuonewa haya kwani muda wa kulindana umepitwa na wakati,” Alisema.


clip_image020_0002

No comments:

Post a Comment