Pages

Pages

Tuesday, February 26, 2013

TANGAZO LA KAZI



ANESA COMPANY LIMITED
P.O.BOX 1295, IRINGA. Mobile +255 719 127 901
Email: anesagroup@yahoo.com, website: www.anesagroup.com

TANGAZO LA KAZI.

Anesa Co.,Ltd ni kampuni ya kitanzania iliyosajiliwa na BRELA na kisha kupewa leseni ya kuendesha biashara mbalimbali kwenye maeneo ya Kilimo(Agriculture), Ufugaji(Livestock), Majengo(Real Estates) na Nyinginezo(General Trading). Kampuni inaendesha shughuli zake katika mikoa ya Iringa, Morogoro na Dodoma. Kwa mwaka 2013 kampuni imepanga kujitanua; hivyo inahitaji wafanyakazi wapya, vijana wenye ari, wabunifu, waaminifu na wenye weledi wa hali ya juu; ili kufanikisha mikakati ya kuitoa kampuni kutoka ngazi moja kwenda nyingine. Kampuni inayofuraha kutangaza nafasi za kazi katika maeneo yafuatayo:

A)MENEJA MAUZO/MASOKO.
SIFA ZA MWOMBAJI
1. Awe na elimu ya diploma au digrii ya biashara au kilimo. Wale wenye diploma na digrii zisizuhusiana na biashara/kilimo wanakaribishwa kutuma maombi ikiwa tu a) Wawe walisoma masomo ya commerce, bookkeeping au Economics katika ngazi ya sekondari b) Katika diploma au digrii walizosoma wawe walisoma na kufaulu unit/course ya eidha ujasiriamali au inayoendana na biashara
2. Awe na umri wa miaka kuanzia 21-35
3. Awe ni mbunifu, mpana katika uelewa wa masuala ya biashara, awe ni mchapa kazi na anayeweza kujisimamia. Mwombaji ajiridhishe kuwa ni mwaminifu na anayeweza kutumia vichache na kuzalisha vingi.
4. Awe na ufahamu wa kutosha kuhusu taratibu za uendeshaji wa makampuni.

B) MUHASIBU
SIFA ZA MWOMBAJI
1 Awe na elimu ya cheti, diploma au digrii katika masomo ya uhasibu.
2 Awe na umri wa miaka 21-35
3 Awe na ufahamu wa kutosha kuhusu taratibu, kanuni na sheria za makampuni
4 Awe na uzoefu ama uelewa wa kinadharia wa kukokotoa mizania ya mirejesho ya kodi za makampuni kwa mujibu wa kanuni na taratibu za TRA.
5 Awe ni mbunifu, mwaminifu, anayejituma na anayeweza kujisimamia mwenyewe.

C) KATIBU MAHSUSI (OFFICE SECRETARY)
SIFA ZA MWOMBAJI:
1. Awe ni wa jinsia ya kike
2. Awe na elimu ya kuanzia kidato cha nne na awe na cheti cha mafunzo ya kompyuta au ya ukatibu mahsusi (secretarial certficate)
3. Awe na umri wa miaka 21-29
4. Awe na uzoefu usiopungua miezi sita katika shughuli zinazofanana ama kukaribiana na nafasi hii.
5. Awe ni mchangamfu, mkarimu, mwaminifu na anayejituma

D) DEREVA
SIFA ZA MWOMBAJI
1. Awe na umri miaka 25-40
2. Awe na leseni class E na kuendelea
3. Awe na uzoefu wa kuendesha magari ya mizigo kwa miaka isiyopungua mitatu
4. Awe mwaminifu na anayeweza kujisimamaia

MISHARA NA MARUPURUPU.
Kampuni ina sera nzuri ambazo zinampa nafsi mfanyakazi kufurahia mazingira ya kazi huku akilipwa mshahara bora na stahiki zinazopendeza.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI.
1. Waombaji wote watume barua za maombi zikiwa zimeambatanishwa na maelezo yao (CV), vivuli vya vyeti pamoja na picha ndogo moja (passport size). Maombi hayo yatumwe kwa “Meneja Utawala” kupitia baruapepe: anesagroup@yahoo.com
2. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 10/Machi/2013, saa 12 jioni.
3. Wale watakaopita katika mchujo wa awali ndio watakaoitwa kwenye usaili.
4. Usaili utafanyika Isimila Hotel, Iringa mjini katika tarehe ambayo itajulishwa kwa wale watakaoitwa kwenye usaili.

IMETOLEWA NA:
MENEJA UTAWALA.
ANESA CO.,LTD,
26/FEBRUARI/2013


No comments:

Post a Comment