Pages

Pages

Monday, February 25, 2013

Rihanna ammwagia sifa za kutisha mpenzi wake Chris Brown

Chris Brown and Rihanna attend the 55th Annual GRAMMY Awards
Chris Brown akiwa na mpenzi wake Rihanna mapema mwaka huu kwenye matukio ya kimuziki.
 
Na Mwandishi Wetu, USA
MWIMBAJI maarufu duniani mwenye maskani yake nchini Marekani, Rihanna, amejikuta akimmwagia sifa mpenzi wake, Chriss Brown kwa madai kuwa anavutia na amebadilika kwa kiasi kikubwa.
 
Wawili hawa walikuwa wapenzi zamani, kabla ya kuingia kwenye mgogoro mzito uliosababisha wawe mbalimbali, ingawa sasa penzi lao limeonekana kuwa moto moto.
Chris Brown and Rihanna in Hawaii
Raha, utamu. Ndivyo wanavyoonekana kusema, Chris Brown na Rihanna walipokuwa ndani ya Hawai Splash wakistarehe zaidi.

Rihanna alisema kuwa hali hiyo inamfanya ajione anafaa zaidi kuwa karibu na mpenzi wake huyo, ingawa kwa sasa wamekuwa wakitawaliwa na wivu wa aina yake, uliosabisha kuzuka kwa minong’ono kuwa wametengana tena kwa madai kuwa Chriss alikuta meseji za mapenzi kwenye simu ya Rihanna.

Rihanna alisisita “Chris amebadilika kwa kiasi kikubwa huku akiwa tofauti na miaka ya 2009 alipokuwa na hasira ingawa kwa sasa tupo kwenye thamani kubwa zaidi,” alisema.
Chris Brown and RihannaHapo sasa. Utamu ehee? Hapa bata tu. Rihanna na Chris

Mwanadada huyo mwenye mvuto wa aina yake aliendeleza kummwagia sifa kwa kumuita Chris kuwa ni mwanaume mzuri na kutangaza upendo wa aina yake juu yake.

No comments:

Post a Comment