Pages

Pages

Monday, February 25, 2013

Mtikisiko Kanisa Katoliki duniani, Padre Mkuu Scotland naye aachia ngazi

Quits ... Cardinal Keith O'Brien
Kadinali Keith O'Brein
 
Na Mwandishi Wetu, Scotland
HALI imezidi kuwa mbaya katika Kanisa Katoliki duniani, baada ya Padre wake, Kardinali Keith O’Brien wa nchini Scotland, kutangaza kuachia ngazi katika wadhifa huo mkubwa kulitumikia kanisa lenye waumini wengi duniani.

Kutokana na hatua hiyo, kiongozi huyo wa kiroho sasa hatakwenda nchini Italia kushiriki kupatikana Papa mpya, baada ya yule Benedict XVI naye kujiuzulu na kuifanya nafasi hiyo iwe wazi na kuleta mtetemko wa aina yake.

Habari kutoka ndani ya Kanisa hilo zinasema huenda kujiuzulu kwa kiongozi huyo wa kirono zimetokana na baadhi yao kukumbwa na kashfa ya kuwavunjia heshima makasisi watatu, hivyo kulazimishwa kuachia ngazi.

Hata hivyo, taarifa hizo zimepingwa na Kardinali huyo, ingawa upekuzi huo umegundua kuwa kujiuzulu kwa kiongozi huyo ni kurudisha heshima ya Kanisa Katoliki kutoka hapa lilipokuwa sasa, huku baadhi yao wakihusishwa kwenye matukio mabaya, yakiwamo yale ya kuwanyanyasa watoto na waumini wao.

Kardinali O’Brien sasa hatapaswa kusafiri hadi Vaticana wiki hii, huku taarifa za shutuma zake zikitajwa kufanyika miaka 30 iliyopita.
Resigned ... Cardinal Keith O'Brien with Prince Philip and Pope Benedict XVI
 Kadinali Keith O'Brien akiwa na Prince Philip and Pope Benedict XVI
 

No comments:

Post a Comment