Pages

Pages

Friday, February 01, 2013

Polisi Kilimanjaro yanasa watuhumiwa wa ujambazi

 
 Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
JESHI la polisi mkoani kilimanjaro linawashikiliwa watuhumiwa wawili wa unyang'anyi wa kutumia silaha.
 
Watuhumiwa hao ni, Mohammed Shani (24) na Emmanuel Jumanne (30), wakazi wa Bomangombe na Sanya juu wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.
ACP-Robart Boaz
Waandishi wa Habari
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, mapema leo, Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, ACP-Robert Boaz amesema kuwa januari 19 mwaka huu majira ya saa kumi jioni huko Bomangombe mtuhumiwa wa kwanza Mohammed Shani alikamatwa akituhumiwa kujihusisha na matukio mbali mbali ya unyanganyi kwa kutumia silaha.

Boaz amesema mtuhumiwa huyo alipohojiwa alikiri kuwa anayo silaha ambayo huitumia kwenye matukio mbali mbali ya uhalifu akiwa anashirikiana na wenzake ambapo aliweza kuwaonyesha polisi sehemu alipokuwa ameihifadhi silaha hiyo.

Kamanda Boaz, amesema kuwa silaha iliyokutwa na mtuhumiwa huyo ni, Bunduki aina ya MARK IV ambayo imefutwa namba za usajili na kukatwa kitako na mtutu pamoja na vifaa vya kutendea uhalifu kama kinyago (mask) 1,maboshore 2, masweta 2,pamoja na risasi 13.

Kamanda Boaz, amesema baada ya kuhojiwa, Mtuhumiwa alimtaja alimtaja mtuhumiwa wa pili Emanuel Jumanne na kuelekeza chumba anamoishi na kilipopekuliwa ilipatikana bunduki moja aina ya shortgun iliyotengenezwa kienyeji na risasi mbili za shortgun, kofia ya jeshi la polisi, boshore 1,begi dogo lililokuwa limehifadhia bunduki hiyo.

Aidha kamanda aliongeza kuwa msako ulianza na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa wilayani Karatu ambapo kwa pamoja walikiri kufanya matukio mbali mbali katika maeneo ya Bomangombe na Sanya juu na Moshi.

Jeshi la polisi mkaoni KilimanjaroWakati huo huo jeshi la Polisi mkoani hapa limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 41,770,000 kutokana na makosa mbali mbali ya usalama wa barabarani katika kipindi cha wiki moja.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz amewaambia waandishi wa habari kuwa kukamatwa huko kulifuatia msako uliofanywa na jeshi hilo ambapo makosa yaliyokuwa yakiangaliwa ni pamoja na mwendo kasi, kuzidisha abiria,magari mabovuna makosa ya pikipiki.

Boaz aliongeza kuwa makosa mengine ni madereva wasiokuwa na leseni,ulevi,kutokuwa na motor vehicle licence,kutokuwa na bima na kupakia abiria kwenye magari ya mizigo.

Amesema kiasi hicho cha fedha kimetokana na tozo za notification  na lengo kuu likiwa ni kupunguza ajali za vifo na majeruhi.

No comments:

Post a Comment