Pages

Pages

Friday, February 01, 2013

The Green Pasture College wafagilia hosteli zao Mwananyamala

Mkuu wa Chuo, Filbert Paschal

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
CHUO cha The Green Pasture College, kimezimwagia sifa hosteli zao zilizopo kwenye eneo la chuo chao kuwa ni nzuri na salama kwa wale wanaopenda kusoma na kukaa hapo hapo.
Jengo la The Green Pasture College linavyoonekana.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Chuo hicho, Filbert Paschal, alipozungumza na Handeni Kwetu leo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya kuanza mwaka wa masomo.

Akizungumza zaidi, Paschal alisema kwamba chuo chao kinachotoa pia elimu ya sekondari, kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, pamoja na elimu ya sekondari kwa miaka 2 (QT), kina hosteli nzuri kwa ajili ya wanafunzi wao.

“Tunaomba wazazi wawalete watoto wao maana hapa ni sehemu nzuri na hakika inasababisha mwamko mkubwa wa wanafunzi kusoma zaidi.

“Kila anayependa kusoma katika chuo chetu akiwa hapa hapa, uwezo huo upo, maana tuna jingo zuri lenye ubora wa hali ya juu, ikiwa ni njia pia ya kuchangia elimu nzuri.

Mbali na kutoa elimu ya sekondari, pia The Green College inayopatikana Mwananyamala Komakoma, inafundisha kozi mbalimbali, ikiwamo ualimu wa chekechekea, masomo ya biashara, Computer na mengineyo.

No comments:

Post a Comment