Pages

Pages

Friday, February 15, 2013

Miss Tanzania 2007 awaropokea wanaoendekeza uzinzi Valentine Day



Mrembo wa Tanzania mwaka 2007, Richa Adhia, katikati, katika kilele cha Valentine Day, kilichoandaliwa na kinywaji cha Baileys.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWANADADA aliyewahi kunyakua taji la Miss Tanzania mwaka 2007, Richa Adhia,  amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kuwajali watu wengine wakiwemo wenye mahitaji maalum kama watoto na wazee  wasiojiweza kimaisha, badala ya kusubiri maadhimisho ya Sikukuu mbalimbali, ikiwamo ile ya Wapendanao, yani Valentine Day kwa minajili ya kufanya uzinzi.
Akizungumza wakati wa kilele cha Siku ya wapendanao iliyoandaliwa na na Kampuni ya Bia ya Serengeti, kupitia kinywaji cha Baileys, katika viwanja vya shoppers jijini Dar es Salaam, Richa alisema huo sio utaratibu mzuri wa kuijali jamii.
 “Siku ya wapendanao ikitumika  kuongeza ari ya kuwasaidia watu wenye mahitaji inakuwa na maana zaidi kuliko kuitumia siku  hiyo kwa mapenzi zaidi kama wanavyofanya baadhi ya watu wanaofanya vitendo hivyo.
“Siku hii itumike kuboresha uhusiano wa wana jamii kwa ujumla na sio kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na watu wengi,” alisema mwanadada huyo.
Aidha, Meneja Masoko wa vinywaji vikali kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti Emilian Rwejuna, alisema wameamua kufanya kampeni hii ili kuamsha ari ya kuwajali na kuwapenda watu na kuwajali kwa kwa ujumla wake.
Alisema kuwa kampuni yao kwa kupitia kinywaji chao cha Baileys imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhamasisha na kutoa chachu na kuahidi kuendelea na mtindo huo.
Kampeni ya msimu wa Siku ya Wapendao ulioandaliwa hiyo ulianza Februari Mosi mwaka huu kwa kupita maeneo mbalimbali ya manunuzi ili kuwahamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kuwanunulia wenzi wao zawadi, ambapo kilele chake kilikuwa juzi Februari 14.

No comments:

Post a Comment