Pages

Pages

Friday, February 15, 2013

Handeni sasa kuipima ardhi yake ili kuepusha migogoro



Muhingo Rweyemamu, kulia akizungumza na simu, wakati anabadilishana mawazo na Benny Mhina, jana.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, amesema kwamba tatizo kubwa linalowasumbua wananchi wake hawajui matumizi bora ya ardhi jambo ambalo wao kama serikali wanajitahidi kuwafikishia ujumbe wa kuwaelimisha.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa New Habari 2006 Ltd, Sinza.

DC Rweyemamu aliyasema hayo na Handeni Kwetu jana jijini Dar es Salaam, akizungumzia kuwa pamoja na mambo mengine, lakini juu ya matumizi bora ya ardhi yanasababisha pia muingiliano mbaya na kilimo kisichokuwa na tija.

Alisema kwamba ofisi yake imejipanga kwa mwaka huu kueneza elimu kwa wananchi wake, hasa juu ya matumizi bora ya ardhi, sambamba kwa kuipima, ikiwa ndio njia rahisi ya kujitambua na kufahamu juhudi za maendeleo.

“Handeni yenye vijiji 112, asilimia kubwa ardhi yake haijapimwa na wananchi wake hawajui namna ya kuitumia au kuiwekeza, ndio maana migogoro imekuwa mingi kwa wilaya yangu.

“Hili najitahidi pamoja na kushirikiana na viongozi wangu kuanzia vijiji, kata, bila kusahau Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, chini ya RC Chiku Gallawa, ambaye amekuwa akifanya ziara mbalimbali kujionea mazingira mazima ya maeneo yetu,” alisema.
 
Utendaji kazi wa Rweyemamu katika wilaya hiyo unaleta matumaini makubwa kwa wananchi wa Handeni, hasa kwa kupambana katika sekta elimu, kilimo pamoja na kuwabana wawekezaji wanaokata mkaa bila kufuata taratibu.

No comments:

Post a Comment