Pages

Pages

Saturday, January 12, 2013

Vijana kuula zaidi Coastal Union

Kikosi cha vijana wa Coastal Union

Na Mwandishi wetu, Tanga
Uongozi wa timu ya Coastal Union B imefungua milango kwa vijana
wanaotaka kujiunga na timu hiyo ya vijana chini ya miaka 20
kujitokeza ili kufanyiwa majaribio.

Akitoa taarifa hizo meneja wa timu ndogo Abdulrahman Mwinjuma
‘Ubinde’ mjini Tanga jana amesema kwakuwa timu ya Coastal Union
B ilionyesha mafanikio makubwa katika michuano ya Uhai mwishoni
mwa mwaka jana kwa kumaliza nafasi ya pili hivyo wachezaji saba
wamepata nafasi katika kikosi cha timu kubwa.

“Mazoezi yanaanza siku ya jumatatu asubuhi tarehe 14 Januari
mwaka huu katika uwanja wa Gymkhana mjini hapa (Tanga), chini ya
kocha wake mkuu Bakari Shime ambae pia alichaguliwa kuwa kocha
mkuu katika michuano ya Uhai.

“Timu ina upungufu wa wachezaji saba ambao walipandishwa kikosi
kikubwa kinachojiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania
bara, kijana yeyote ambae ana umri chini ya miaka 20 akitaka
kufanyiwa majaribio awasiliane na mimi kwa namba (0654851612)
ama aje katika klabu ya timu iliyo barabara ya 11 Tanga,”
alisema Ubinde.

Wachezaji saba ambao walipanda timu kubwa ambayo wiki iliyopita
ilikuwa Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi na
kutolewa katika hatua ya makundi ingawa haikupoteza mchezo hata
mmoja ni; aliekuwa golikipa bora wa michuano ya Uhai Mansour Mansour, AbdiBanda, Ally Nassor, Hussein Twaha ‘messi’, Hamad juma, Nzara
Ndaro, na Ramadhan Shame ‘Batista’.

No comments:

Post a Comment