Mchungaji William Mwamalanga
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Kamati ya Maadili ya Viongozi wa Dini, ambaye
pia Mchungaji wa Kanisa la Pentekost, mkoani Mbeya, William Mwamalanga, amesema
hali ni mbaya wilayani Handeni mkoani Tanga, kufuatia njaa na ukosefu maji safi
na salama.
Akizungumza na Handeni Kwetu jana jijini Dar es Salaam,
Mwamalanga, alisema kwamba njaa ni kali kiasi kwamba watu wengine wanakula
maembe na mboga mboga.
Alisema baada ya kusikia hali hiyo kwenye vyombo vya habari,
akiwa kama kiongozi wa dini, alilazimika kufunga safari hadi katika wilaya hiyo
ili kuangalia balaa hilo.
“Hali ni mbaya, hivyo naomba wadau sasa waingilie kati kwa
kunusuru watu ambao watapoteza utu na uhai wao kwasababu ya njaa, ambayo ndio
tishio kubwa kwa wakazi wa Handeni.
“Nimetoka Mbeya kwa ajili ya kwenda Handeni na kukaa kwa
wiki mbili nikitembelea sehemu kubwa ya wilaya, hivyo nimejionea mwenyewe na
watu wajuwe hali si nzuri,” alisema Mwamalanga.
Hata hivyo serikali kwa kupitia Mkuu wa Wilaya ya Handeni,
Muhingo Rweyemamu na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa, walitangaza
kupelekewa chakula cha bei rahisi, ambapo wananchi wao watalazimika kununua kwa
bei isiyozi 750 hadi 900.
No comments:
Post a Comment