Pages

Pages

Friday, January 04, 2013

Serikali yaombwa kusaidia wajasiriamali

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SERIKALI kwa kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, imeombwa kuwasaidia wajasiriamali kwa kuwawezesha kwa mikopo ili waweze kufanya kazi za kwa ufanisi na kuongeza pato la Taifa.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Grace Products, Elizabeth Kilili, alipozungumza na Habari na Matukio jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza zaidi, Elizabeth alisema kwamba wapo wajasiriamali wadogo na wakubwa ambao kwa kiasi fulani wanaweza kusonga mbele kama serikali yao itawasaidia hata kwa kuwafanikishia suala zima la mikopo.
Alisema watu wengi wamekuwa wakishindwa kufanya biashara zao kwa kiwango cha Kimataifa, huku changamoto kubwa ikiwa ni upatikanaji wa vifaa vya kuwafanyia kazi kutokana na kukosa uwezo mkubwa kifedha.
“Tunaiomba serikali kuwa makini katika hili la kusaidia wafanyabiashara wa Tanzania, wakiwamo wale ambao uwezo wao ni mdogo na hawana uwezo au sifa za kukopesheka kama wanavyofanya baadhi yao hapa nchini.
“Kwa mfano mimi nafanya biashara ya kutengeneza bidhaa zangu mbalimbali ikiwamo ya sabuni ya kuogea ya Grace Manjano, Shampoo na nginginezo zenye nembo ya Grace Products Ltd, lakini ukosefu wa fedha ni tatizo kwangu,” alisema.
Elizabeth ni miongoni mwa wajasiriamali wenye uchu wa mafanikio, huku bidhaa zake zikianza kufanya vizuri na kuvuka mipaka, jambo ambalo linaweza kuipatia nchi mafanikio makubwa zaidi kama atawezeshwa na serikali yake.

No comments:

Post a Comment