Rais wa FM Academia, Nyosh el Sadaat
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS wa bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ Nyosh El Sadaat, amekanusha
uvumi ulionea hapa nchi kuwa ndiye aliyemroga mwimbaji Alpha Kabeza.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Nyosh alisema hawezi
kufanya kitu kama hicho na anashangazwa na taarifa hizo.
“Mimi sijui ni kwanini wanasema hivyo, ila
sijamroga Kabeza na kwanini nimroge, niko Ngwasuma tangu zamani, yeye amekuja
mwaka 2006, sasa namroga ili iweje?,” alisema Nyosh.
Kabeza, ambaye mwanzoni aliondolewa kwenye bendi
ya Ngwasuma kutokana na kuwa msumbufu, amekuwa kama mtu aliyechanganyikiwa kwa
muda sasa, huku baadhi ya mashabiki wakidai kuwa amerogwa na Nyosh, kutoka na
uwezo wake wa kuimba vizuri.
Bendi hiyo wiki hii itaendelea na ratiba zake
kama kawaida, ambapo Jumatano watakuwa New Maisha Club, Jumamosi watapiga
Ukumbi wa Kijiji cha Makumbushi na Jumapili kumaliza kwa bonanza kwenye Ukumbi
wa New Msasani Club.
No comments:
Post a Comment