Bondia
Antony Mathias (kushoto) akitunishiana misuri na Fadhili Majia baada ya kupima
uzito, Dar es salaam kwa ajili ya mpambo wao kesho utakaofanyika katika
ukumbi wa CCM Tandale.
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA
Hassan Mandulla na James Martin wanatarajia kupanda ulingoni kesho Jumapili,
Januari 27 katika Ukumbi wa wa CCM Tandale, jiji Dar es salaam.
Muandaaji
wa pambano hilo, Waziri Rosta, amesema mabondia hao wamepima uzito leo
pamoja na kujua afya zao kwa ajili ya kivumbi hicho cha wanamasumbwi.
Mbali
na mabondia hao, pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kama vile, Fadhili
Majia, atakayekipiga na Anthon Mathias,
Kalama
Nyilawila na Athumani Pendeza.
Michezo mingine ni Shabani Kilumbelumbe na Mwaite Juma, huku Charles Mashali akivaana na Adam Ngange, wakati Julius Noro akivaana na Abdallah Luwajempambano, Rajabu Tumaini na Daudi Anton, huku Rashid Mohamed akipigana na Eliman Richard, bila kusahau Rashid Hamisi atakayepigana na Omary Shabani.
Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.

Super D, alisema mbali na michezo ya
nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Juan Emanuel Marquez, Floyd
Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo ya tamasha
lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.
“Katika muendelezo wa kuwafunza watu
ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya
michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha
letu na Kinyogoli Foundition,” alisema.
Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi
ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia
njia hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia
mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye
dvd hizo.
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana.
No comments:
Post a Comment