Anna Abdallah, Mbunge wa Viti Maalum na Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho.
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HALI
inaendelea kuwa mbaya mkoani Mtwara, baada ya baadhi ya wananchi kufanya vitendo visivyokuwa vya kiungwana kwa kuchoma moto na kuharibu mali mbalimbali, kwa madai kuwa madereva wa bodaboda wanaonewa katika shughuli zao.
Leo tayari wananchi
hao wamechoma moto nyumba ya Mbunge wa Viti Maalum, Anna Abdallah, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho, sambamba na kuchoma ofisi ya
Halmashauri, Ofisi ya CCM na vitu vingine, ikiwa ni muendelezo wa kadhia hizo
mkoani Mtwara.
Wakati
hayo yakiendelea, jana katika mkoa huo pia kuliwa na tatizo kama hilo, baada ya
nyumba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia.
Habari
kutoka kwa mtu aliyekuwa mkoani Mtwara zinasema kwa ujumla wananchi wengi
wamekumbwa na taharuki kufuatia harakati hizo zilizopamba moto, hasa chanzo
chake kikiwa gesi, ingawa jana kuliibuka tena sakata la ushirikina, kwa madai
kuwa nyumba ya diwaniwa Kata ya Chikongola, Manispaa ya Mtwara Mikindani,
Mohamed Chehako kuwa inahifadhi wachawi.
Sakata
hilo lililazimisha polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi
waliovamia nyumba hiyo.
Juhudi
za kupata matukio yanayoendelea mkoani Mtwara leo zinaendelea, ikiwa ni pamoja
na kuendelea kuchambua kwa undani sakata hilo linalokolea kila siku ya Mungu,
hivyo kuweza kuwagawa wananchi.
No comments:
Post a Comment