Ngowi akiwa na mwamuzi Jaap Van Niewenhuizen wa Afrika ya Kusini.
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
RAIS
wa IBF katika Bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Onesmo
Ngowi, atasimamia pambano la ubingwa wa Dunia la vijana katika jiji la
Johannesburg nchini Afrika ya Kusini, Februari 15, kati ya Mkongo, Illunga
Mukaba atakayekipiga na Gogita Gorgiladze wa nchini Georgia.
Katika
taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari, Mabondia hao wenye wiwango
vinavyolingana Georgita (12) na Makaba (12) watapambana kugombea mkanda wa
vijana wa wa Dunia (Youth Title) wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF)
katika uzito wa Cruiserweight tarehe 15 February, 2013.
Mpambano
wa wawili hawa utafanyika katika hoteli ya nyota 5 ya Emperors Palace in
Kempton Park, Gauteng katika jiji la Johannesburg, nchini South Africa.
Ngowi
kama kamishna mkuu wa pambano hilo atasaidiwa na maofisa wafuatao: Refarii: Wally Snowball (Afrika
Kusini). Jaji Namba moja:
Simon Xamlashe (Afrika Kusini), Jaji namba mbili: Manuel Maritxalar
(Spain) na Jaji namba tatu: Jaap
Van Niewenhuizen (Afrika ya Kusini).
Mpambano
huu ni kati ya mapambano zaidi ya 100 ya IBF yatakayofanyika katika bara la
Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika kipindi cha mwaka huu wa
2013 chini ya mradi wa IBF wa Utali wa
Michezo.
No comments:
Post a Comment