Pages

Pages

Friday, January 04, 2013

Mafuriko yaikumba Sindeni wilayani Handeni

Na Mwandishi Wetu, Handeni
NYUMBA zaidi ya 37 zimekumbukwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa kunyesha mwishoni mwa wiki katika tarafa ya Sindeni, wilayani Handeni mkoani Tanga.
Mbali na nyumba hizo, pia bwawa muhimu linalotumiwa na wakazi wa Sindeni la Msonera, nalo limesombwa na kuwaacha njia panda wananchi wa Sindeni.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mvua hiyo imenyesha kwa zaidi ya saa tatu na kuleta kadhia hiyo, jambo linalowafanya wananchi hao wahitaji msaada mkubwa kutoka serikalini.
Mwandishi wetu aliyekuwa wilayani Handeni, alitupasha kuwa baada ya mvua hiyo kunyesha, bwawa lilisombwa pamoja na nyuma 37, huku ikidariwa kuwa zaidi ya mifugo elfu 70,000 itaathiriwa kwa kuharibiwa kwa bwawa hilo.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu (pchani) , alithibitisha kutokea kwa mvua hiyo iliyosomba bwawa hilo na kusema wanahitaji msaada kutoka serikali kuu kwasababu tatizo hilo sio la watu wa Handeni peke yao.
“NI habari mbaya kwetu wote, maana mvua hii iliyonysha kwa saa kadhaaa imeleta balaa na kuziacha kaya katika mashaka makubwa, sambamba na mifugo ambayo huenda ikawa kwenye wakati mgumu kama hakutakuwa na njia nzuri ya kusaidia.
“Sisi kwa pamoja tutajaribu kushirikiana kwa karibu na wenzetu wa serikali, ikiwamo ofisi ya Waziri Mkuu ili tupate msaada zaidi,” alisema Rweyemamu.
Licha ya mvua kuwa jambo la muhimu kwa watu wote duniani, lakini wakati mwingine huwa inaleta madhara na kuziacha kaya katika wasiwasi mkubwa hasa pale inapoharibu miundo mbinu mbalimbali na hata mafuriko yanayoziacha kaya njia panda.

No comments:

Post a Comment