Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako
Na Mwandishi Wetu, Uturuki
TIMU ya Yanga, inatarajia kuondoka nchini Uturuki kesho
mchana
baada ya kumaliza kambi yao ya wiki mbili waliyoweka nchini
kwa
ajili ya kujiandaa na ligi ya Tanzania Bara, hatua ya
mzunguuko
wa pili.
Ligi hiyo imepangwa kuendelea tena baadaye mwezi huu, huku
timu
mbalimbali zikijiandaa kwa ajili ya kufanya vizuri katika
patashika hiyo.
Yanga inarejea Tanzania, huku ikiwa na kumbukumbu ya
kumaliza
vibaya mechi zao za Kimataifa za kirafiki, baada ya kukubali
kichapo cha bao 2-0 dhidi ya Emmen FC inayoshiriki ligi
daraja
la kwanza nchini Uholanzi.
Mechi hiyo ya mwisho ilichezwa katika Uwanja wa Arcuda
Football uliopo Antalya, huku ikileta huzuni kwa wachezaji na mashabiki wa
Yanga.
Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, amesema kuwa Yanga baada
ya kuondoka mchana wa siku ya Jumapili ya Januari 13, itaingia jijini Dar es
Salaam alfajiri ya siku ya Jumatatu.
Kufuatia kipigo hicho cha bao 2-0, kocha wa Yanga, Ernest
Brandts, aliumizwa na matokeo huku akisema timu yake ilicheza vizuri, ingawa
walishindwa kuwa makini zaidi na kufungwa mabao hayo.
Kwa mujibu wa Kizuguto, Yanga inayofanya mazoezi ya mwisho
leo mchana nchini hapa, itaanza safari ya kurudi Tanzania siku ya jumapili
mchana, ambapo itafika Dar es salaam alfajiri ya siku ya Jumatatu.
Kikosi kilichoanza kipindi cha kwanza: Said Mohamed, Juma
Abdul,
Stephano Mwasika,
Nadir Haroub 'Cannavaro', Shadrack Nsajigwa,
Nurdin Bakari, Saimon Msuva, Frank Domayo, Geroge Banda,
Nizar
Khalfani, Haruna
Niyonzima.
Kikosi cha kipindi cha pili: Yusuph Abdul, Mbuyu Twite,
Oscar
Joshua, Ladislaus Mbogo, Kelvin Yondani, Athuman Idd 'Chuji,
Godfrey Taita, Omega Seme, Didier Kavumbagu, Jerson
Tegete/Rehani Kibingu, David Luhende.
No comments:
Post a Comment