Pages

Pages

Thursday, January 31, 2013

Taasisi yajiingiza kupigania maisha ya watu wenye ulemavu

Katibu wa Taasisi ya The John Mashaka, Rabia Bakari, akizungumza kwa ajili ya kufungua mkutano wa waandishi wa habari na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu ili kujadili kwa pamoja ustawi wa walemavu na wengine wasiojiweza. Picha zote kwa hisani ya www.burudan.blogspot.com
Baadhi ya watu wanaotafsili lugha za alama wakiendelea na kazi hiyo wakati wa mkutano
Baadhi ya wawakilishi wakisikiliza kwa makini
Mwenyekiti wa TUSPO Bw. E LLEZER Mdakima kushoto akizungumza wakati wa mkutano huo wengine kulia ni Mjumbe wa Taasisi ya The John Mashaka Bi, Latifa Masasi na Katibu wa taasisi hiyo, Rabia Bakari.

Chid Benz, Amini, Tunda Man kukamuana na Extra Bongo kesho

Chid Benz


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WASANII wane wa muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva, Chid Benz, Amini, Synag na Tunda Man, wamepangwa kufanya shoo ya wiki nne za zawadi inayoandaliwa na Extra Bongo, itakayofanyika Ijumaa, katika Ukumbi wa Ikweta Grill, Temeke.

Kufanyika kwa onyesho hilo ni maalum kwa ajili ya kutoa burudani kwa wapenzi wa muziki nchini, huku ikitoa zawadi mbalimbali, ikiwamo 150,000 na elfu 50,000, katika shoo iliyofanyika Meeda wiki iliyopita.

Akizungumza na Handeni Kwetu, Mkurugenzi wa bendi hiyo, Ally Choki, alisema kuwaita wasanii hao wa kizazi kipya ni kuongeza hamu ya utoaji wa burudani kwa wapenzi wao.

Alisema kila kitu kinaendelea vizuri kwa ajili ya wanamuziki wa bendi yake na wasanii hao wa Bongo Fleva kufanya mambo katika shoo hiyo.

“Tunafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa burudani ya wiki nne za zawadi inakuwa ya aina yake na watu wapate raha wanapokuwa ukumbini.

“Naamini kila kitu kitakuwa sawa, maana waimbaji hao tumeshafikia muafaka na wamekubali kuja kutoa burudani katika tukio hilo la Ijumaa,” alisema.

Onyesho hilo la Ijumaa atakosena msanii Linah, ambaye nafasi yake imejazwa na msanii Chid Benz, ambaye naye amejigamba kufanya makubwa katika shoo hiyo.

Vita ya ukahaba Tanzania, wakamatwe na wateja wao


Changudoa akizungumza na mteja wake, katika moja ya mitaa ya jiji la Dar es Salaam.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TANZANIA imezidi kuingia kwenye vitendo viovu vikiwamo vya ukahaba, jambo linalosababisha serikali kuliangalia hilo kwa kina.
 
Hawa walikutwa mida mibovu, nao eti wapo kazini.

Leo tunashuhudia baadhi ya sehemu zenye mwingiliano mkubwa wa watu wengi, serikali inapenyeza jicho lake kiasi cha kuwakamata au kuwakimbiza akina dada wanaofanya vitendo vya kuuza miili yao.

Kim aita wachezaji 21 wa Stars, Kaseja ndani

Kocha wa Stars, Kim Poulsen.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).


Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.


“Itakuwa mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.


“Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.


Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.


Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).


Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Hifadhi ya Taifa Serengeti yanyakua tuzo ya Kimataifa ya Utalii

Wildbeest in the plains of Serengeti National Park, the winner of 2013 International Award for the Tourist, Hotel and Catering Industry(3)

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imeteuliwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Kimataifa ya Utalii, Hoteli na Huduma za Vyakula kwa mwaka 2013. Uteuzi huu umefanywa na kamati ya uteuzi ya tuzo hizo baada ya Serengeti kukidhi vigezo vilivyowekwa na waandaaji wa tuzo hizo.

Taarifa iliyotumwa na Meneja Uhusiano wa Hifadhi za Taifa Tanzania, Paschal Shelutete ilisema kuwa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) litapokea tuzo hiyo itakayotolewa kwa Serengeti katika hafla maalum itakayofanyika mjini Madrid nchini Hispania tarehe 30.01.2013. Tuzo hizi huandaliwa na taasisi maarufu duniani inayofahamika kama Global Trade Leaders’ Clubinayohusisha makampuni yapatayo 7000 duniani. 

Tuzo hii ilianzishwa kwa ajili ya kutambua na kuenzi michango inayotolewa na taasisi na makampuni yanayojihusisha na utalii, hoteli pamoja na huduma za vyakula kama njia ya kuthamini mchango na kuhamasisha wale wote wanaofanya kazi katika sekta hii ambayo ni muhimu katika maendeleo ya uchumi wa nchi husika.

Hafla ya utoaji wa tuzo za mwaka huu itahudhuriwa na wadau wa shughuli za utalii kutoka nchi zipatazo 40 duniani na zitaambatana na Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii yanayofanyika kila mwaka mjini Madrid, maarufu kama FITUR ambayo Tanzania ni mshiriki.

Hifadhi ya Serengeti ni hifadhi kongwe nchini ambayo ilianzishwa miaka zaidi ya hamsini iliyopita na ambayo pia ni Eneo la Urithi wa Dunia. Hifadhi hii ni maarufu kwa Nyumbu wahamao kila mwaka katika mzunguko unaohusisha nchi mbili za Tanzania na Kenya. Mzunguko huu wa wanyama wahamao unaaminika kuwa ndio pekee uliobakia ulimwenguni unaohusisha wanyama wakubwa wa ardhini.

Kutolewa kwa tuzo hii ambayo ni heshima kwa TANAPA na nchi kwa ujumla ni matokeo ya sera nzuri za uhifadhi zinazosimamiwa na TANAPA katika kuhakikisha kuwa maeneo yaliyotengwa kisheria kama Hifadhi za Taifa yanaendelea kuhifadhiwa vema kwa ajili ya vizazi vijavyo lakini pia kuhakikisha kuwa viwango vya huduma za utalii katika hifadhi zinakuwa za kiwango cha kimataifa ili kuhudumia wageni watokao sehemu mbalimbali ulimwenguni.


 

Dkt. Asha Rose Migiro apewa tena ulaji na Rais Kikwete

Dkt. Asha Rose Migiro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini leo, Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.

Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Aidha, Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
30 Januari, 2013


Wednesday, January 30, 2013

Banza Stone wa zamani atokea tena Extra Bongo



Banza Stone anavyoonekana sasa Extra Bongo.
Huyu pia ni Banza Stone, alipotoka kuumwa.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WADAU wa muziki wa dansi hapa nchini, wamepongeza maendeleo ya afya ya mwanamuziki nguli, Ramadhani Masanja Banza Stone, anayefanya kazi na swahiba wake, Ally Choki, katika bendi ya Extra Bongo, Next Level.

Banza Stone alikuwa kwenye matatizo mengi ya kiafya, hali iliyowafanya baadhi ya watu wenye roho nyepesi kumzushia kifo kutokana na hali yake.

Hata hivyo, baada ya kuitwa na Choki katika bendi hiyo, Banza Stone amekuwa kwenye kipindi kizuri cha afya yake kuimarika, jambo linaloleta tumaini kubwa.

Mtu wa karibu na bendi hiyo, aliiambia Handeni Kwetu juzi katika bonanza lao linalofanyika kila Jumapili, Magomeni kuwa wamekuwa wakimshauri sana mwanamuziki huyo ajilinde na matumizi mabaya ya ulevi hali itakayomuweka njia panda.

“Afya yake inachangiwa na ulinzi anaopewa pamoja na ushauri hapa Extra Bongo, ukizingatia kwamba hapo kabla alikuwa kwenye wakati mgumu kiasi cha kutabiriwa kifo.

“Hata yeye mwenyewe alishakata tama, lakini kwa mwendo huu mambo ni mazuri, maana ana nguvu zake pamoja na uwezo wa kupaza sauti katika shoo za Extra Bongo,” alisema mpashaji huyo.

Banza Stone anakumbukwa na uwezo wake wa utunzi na uimbaji, huku wadau wakikumbuka jinsi alivyofanya mambo katika nyakati mbalimbali, hasa kipindi cha kuwika kwa Choki, Mwinjuma Muumini nay eye mwenyewe.

Banza pia amewahi kuwika na bendi mbalimbali, kama vile The African Stars, Twanga Pepeta, TOT na nyinginezo alizojiunga nazo katika kipindi chote cha maisha yake ya muziki na kutoa vibao mbalimbali kama vile Mtu Pesa, Kisa cha Mpemba, Majungu sio Mtaji na nyinginezo.

Idd Azan mgeni rasmi pambano la Kaseba na Maneno



Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MBUNGE wa Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idd Azan, amepangwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la Ubingwa wa Taifa, litakalowakutanisha Japhet Kaseba na Ramadhan Maneno, liliopangwa kufanyika Machi 2 mwaka huu, katika Ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa, jijini Dar es Salaam.

Pambano hilo ndilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa masumbwi, likiwakutanisha wakali wa ndondi, akiwamo Kaseba, aliyewahi kuwika pia kwenye ngumi za mateke.

Akizungumza na Handeni Kwetu, Kaseba alisema kuwa pambano lao litahudhuriwa na mbunge wa Kinondoni, akiwa na shauku ya kutaka kujua nani mkali.

Alisema katika masumbwi hayo, kila mmoja anataka kuonyesha makali yake, huku yeye akiwa na hamu zaidi ya kuonyesha kwanini anakimbiwa na mabondia wengi.

“Nimekuwa nikikimbiwa sana na mabondia hapa nchini, hivyo naamini katika pambano hili ambalo mgeni rasmi atakuwa mbunge wa Kinondoni, nitaonyesha ukweli huo.

“Kila kitu kinaendelea vizuri kuelekea katika patashika hiyo itakayokutanisha pia mabondia wengine wenye uwezo, akiwamo Mtambo wa Gongo na wengineo,” alisema.

Mwaka jana Kaseba alishindwa kupigana na Francis Cheka, licha ya kutangazwa mno na wadau wa ngumi na kupangwa kufanyika katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala.