Pages

Pages

Saturday, December 22, 2012

Elizabeth: Watanzania wengi wana magonjwa ya ngozi


Mkurugenzi wa Grace Product, Elizabeth Kilili akiwa ofisini kwake.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa Kampuni ya Grace Product Ltd, ya jijini Dar es Salaam, Elizabeth Kilili, amesema kwamba Watanzania wengi wana magonjwa ya ngozi na kuhatarisha afya zao.

Elizabeth ameyasema hayo muda mfupi alipokuwa akizungumza na Handeni Kwetu ilipotembelea ofisini kwake, Ukonga na kuonyesha bidhaa zake zinazopambana na magonjwa ya ngozi.

Akizungumzia hali hiyo, Elizabeth alisema kwamba kutokana na hilo, bidhaa zake zinaweza kuondosha kabisa magonjwa hayo, yakiwamo mapunye, mba, muwasho na yote yanayosababisha ngozi zishindwe kuwa kwenye mwonekano mzuri.

Alisema bidhaa zake kama vile Shampoo, loation na sabuni yake inayojulikana kama Grace Manjano Soap zinazopatikana madukani kote ni nzuri kiasi cha kuondoa matatizo hayo.

“Watanzania wengi wana matatizo ya ngozi kutokana na mazingira au shughuli zetu pamoja na wengineo kuathiriwa zaidi na bidhaa walizowahi kutumia.

“Kwasababu hiyo, bidhaa zangu zote ambazo kwa sasa zipo sokoni zinba uwezo wa kuondoa matatizo hayo na kuwafanya watu wawe kwenye afya njema,“ alisema.

Kwa mujibu wa Elizabeth, bidhaa zake nyingine anazotengeneza ni pamoja na sabuni ya kufulia na kuoshea vyombo inayoitwa liquid Soap, Disinfectant inayotumika kusafisha nyumba na choo.



No comments:

Post a Comment