Pages

Pages

Saturday, December 22, 2012

Diamond na Dimpoz kumenyana Dar Live




 Diamond na Ommy Dimpoz kwenye pozi

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WASANII mahiri wa miondoko ya kizazi kipya nchini Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Ommy Diampozi, wanatarajia kupanda jukwaani kutoa burudani katika Sikukuu ya Krismasi, kwenye Ukumbi wa Dar Live, uliopo Mbagala, Zakheem jijini Dar es Salaam.

Diamond na Dimpoz, watakutana kwa mara ya kwanza katika ukumbi huo, ikiwa ni kusherehekea pamoja na wadau wa muziki huo pamoja na mapambano ya ngumi.

Onyesho hilo maalum la kusherehekea Krismasi, limeandaliwa na  Kampuni ya Global Publishers na Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBO), chini ya Rais wake, Yasin Abdallah ‘Ustadhi’.

 Akizungumza kuhusu onyesho hilo, Diamond alisema ni faraja kwake kujumuika na mashabiki wake katika ukumbi wa Dar Live na kuwapa burudani, huku akiwaomba kujitokeza kwa wingi katika onyesho hilo.

“Kwanza nawashukuru mashabiki wangu wa kuniunga mkono na kununua kazi zangu, nawaomba mjitokeze kwa wingi Dar Live, mshuhudie nitakavyomfundisha kazi mdogo wangu Diampoz, mimi ni kaka yake na aliyetangulia katangulia tu,” alisema Diamond huku akishangiliwa na masjhabiki waliofurika nje ya viwanja vya Karume, Dar es Salaam.

Katika onyesho hilo pia kutakua na mapambano ya ngumi, ambapo bondia Mbwana Matumla wa Tanzania, atazichapa na David Charanga kutoka Kenya, katika pambano la raundi 6, huku Mada Maugo wa Tanzania, akizichpa na Yiga Juma kutoka Uganda katika pambano la raundi 6 pia.

Katika pambano jingine, Chupaki Chipinda, atazichapa na Bahati Mwafyele katika pambano la raundi 6, aambapo pia kutakua na burudani kutoka kwa kundi la muziki wa dansi la Extra Bongo, pamoja na msaniii wa Kizazi Kipya kutoka TMK Wanaume, Juma Nature.  
Katika onyesho hilo la aina yake, kiingilio kitakua Sh 10, 000.

No comments:

Post a Comment