Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa
Wanawake Tanzania (TWFA) unatarajia kufanyika Desemba 19 mwaka huu mjini
Morogoro.
Taarifa iliyotumwa Handeni Kwetu na Mwenyekiti wa
Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala, ilisema uchaguzi huo utatanguliwa na
Mkutano Mkuu wa TWFA.
Wajumbe wapiga kura wote wa mikoa iliyofanya uchaguzi
wake na kutoa taarifa za uchaguzi wao ofisi za TWFA wanatakiwa kufika Morogoro
siku moja kabla (Desemba 18 mwaka huu).
Wagombea waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi ni kama ifuatavyo; wanaowania
uenyekiti ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy. Rose Kissiwa ni mgombea
pekee wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Wanaowania ukatibu mkuu ni Amina Karuma na Cecilia
Mkafu. Nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) inagombewa na Zena Chande pekee baada ya Furaha Francis kujitoa
kutokana na sababu za kifamilia.
Sophia Charles na Triphonia Temba wanawania nafasi ya
ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho.
Wagombea Rahim Maguza, Macky Mhango na Rose Msamila
wameondolewa kwa kushindwa kikidhi matakwa ya Katiba ya TWFA Ibara ya 28(2).
No comments:
Post a Comment