Mkurugenzi wa Giraffe Ocean View, Charles Bekoni
Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
KATIKA maendeleo ya sanaa yanayoendelea kutukia katika ardhi
ya Tanzania,
hakika yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na ushirikiano na moyo wa wadau wake.
Wadau hao wanafanya hivyo kwa kuamini kwamba itachangia kwa
kuwakomboa wasanii na sanaa yao,
jambo ambalo litawapa mwanga wa kujinufaisha.
Wapo wengi mno. Na kila mmoja ana umuhimu wake na nafasi
yake, katika kuitangaa sanaa hiyo.
Warembo wakijiachia katika hoteli ya Giraffe Ocean View, Dar es Salaam
Miongoni mwao ni Giraffe Ocean View Hoteli, iliyopo Mbezi
Beach, jijini Dar es Salaam, ambayo kwa hakika inafanya juhudi kubwa kuwasaidia
sanaa na wasanii nchini.
Hiyo inatokana na hoteli hiyo kuweka utaratibu mzuri wa
wasanii kupiga picha za kazi zao katika hoteli hiyo. Utaratibu huo kwa hakika
unaleta tija.
Warembo wakijiachia maeneo ya Giraffe Ocean View
Wasanii wanafanya mazuri kwa ushirikiano huo, ambao umewekwa
na hoteli hiyo ya kisasa inayomilikiwa kwa kiasi kikubwa na Watanzania.
Katika sanaa ya maigizo, wasanii mbalimbali wamekuwa
wakifanya sanaa zao hapo, hasa kwa kurekodi filamu zao hapo na kuwa kwenye
kiwango cha juu mno.
Ukaicha wasanii wakubwa, hata wanaochipukia nao hawanyimwi
fursa hiyo, ukizingatia kwamba lengo la hoteli hiyo ni kuwapa nafasi wasanii
kuonyesha uwezo wao na kujipatia mafanikio.
Kwa kipindi kirefu mwaka jana, kundi la Dar Talents, maarufu
pia kwa jina la Bongo Hood, lilikuwa likirusha mchezo wao wa Cinderela,
ulioandaliwa kwa kiasi kikubwa na maeneo ya Giraffe.
Hii ni njia nzuri ya kuendeleza wasanii wachanga. Wasanii
ambao kila kinachopita mbele yao,
ni changamoto, inayoweza kuwakwamisha.
Wapo waliokuwa wakijidanganya kwamba ili uweze kurekodi
katika hoteli mfano wa Giraffe, ni kuwa na jina kubwa au uwezo mkubwa wa
kifedha.
Kama hao wapo
basi wanajidanganya.
Tena wataendelea kujidanganya, kama hawatatoa woga na
kuamua kujitoa kama wanataka kufanya kazi
nzuri.
Hoteli za kisasa, hasa zinazomilikiwa na Watanzania, zinaweza
kuwasaidia Watanzania kwa ujumla, hasa kwa kuwashirikisha katika matukio
makubwa ya kisanaa.
Huo ndio ukweli. Ukiangalia wasanii wakubwa waliofanikiwa
hapa nchini, mara kadhaa hupenda kutumia hoteli hiyo kwakujua ni mahali pazuri.
Hata hivyo haitoshi, bado sanaa ya urembo nayo inategemea
uwepo wa hoteli hiyo. Ingawa zipo hoteli nyingi hapa nchini, lakini kwao
Giraffe wameona ndio kila kitu.
Inajitoa kwa moyo na nia ya kufanya nao kazi. Ndio, maana
tunashuhudia ni jinsi gani Miss Tanzania, chini ya Mkurugenzi wake, Hashim
Lundenga, anapoitumia hoteli hiyo katika kuanbdaa shindano lenye mvuto.
Kwa miaka kaadhaa, Miss Tanzania
wamekuwa wakiweka kambi yao
hapo, ama kupata msaada wa aina mbalimbali, jambo linalotakiwa kupongezwa na
wadau wote.
Mchango wao katika sanaa ya urembo ni mkubwa, huku nikiamini
kwamba Miss Tanzania
wasingeweza kuulipa kama wangetakiwa walipe
kwa fedha.
Kila mmoja anafahamu gharama za kumlaza mrembo mmoja katika
hoteli kubwa kama Giraffe Ocean View. Kama
hivyo ndivyo, vipi kwa warembo wa Tanzania
nzima wanaoshiriki shinda no hilo
la kitaifa.
Ukiacha Miss Tanzania, ni Giraffe pia walioamua kulibeba kwa
asilimia kubwa shindano la Unique Model.
Shindano hili lililoandaliwa kwa mara ya kwanza mwaka jana, liliweza
kufikia hatua nzuri, baada ya kuwezeshwa kwa kiasi kikubwa na wadau hao wa
Giraffe.
Kama hivyo ndivyo, ni vipi mimi kama
mdau nitashindwa kutumia walau robo tu, kuwashukuru Giraffe Hoteli, chini ya
Mkurugenzi wake, Charles Bekoni.
Hakika siwezi. Na kila mwenye nia ya kuitangaza vyema sanaa
ya Tanzania,
lazima atapenda kuwashukuru wadau hao, maana mchango wao ni mkubwa.
Bila hata kuangalia katika shindano la Dunia warembo wetu
hupata kitu gani, ila katika ngazi ya kitaifa, hakika ni mchango mkubwa mno
katika shindano la urembo.
Hivi karibuni, Mkurugenzi huyo wa Giraffe Ocean View, Bekoni,
aliwahi kuliambia Handeni Kwetu kuwa lengo lao ni kuwapa mwanga na fursa
wasanii wa Tanzania.
Hoteli hiyo itaendelea kuwaunga mkono wasanii na sanaa yao kwa pamoja, huku
akisifia utaratibu huo kuwa ni sehemu ya kujitanua kibiashara.
“Biashara yetu inakuwa nzuri kama
tutakuwa karibu na jamii, hivyo naamini bado tuna nia ya dhati ya kupiga hatua
kutoka hii na kwenda nyingine.
“Naamini tutafanikisha ndoto zetu, ukizingatia kwamba
tumepigania kuiweka hoteli hii katika kiwango cha juu mno kutokana na kujengwa
vizuri pamoja na kutoa huduma nzuri na ya kuaminika,” alisema Bekoni.
Giraffe ni miongoni mwa hoteli za kisasa zinazowapa fursa
wasanii kurekodi kazi zao, akiwamo marehumu Steven Kanumba, aliyefariki mapema
mwaka huu.
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment