Pages

Pages

Wednesday, December 19, 2012

Sijafurahishwa na matangazo ya REA


Maoni ya Handeni Kwetu
GAZETI la Mtazania Jumapili la Desemba 16 lilichambua kwa kina makala iliyokwenda kwa jina la Sera ya Umeme vijijini ipo kwenye makaratasi.
Kambi Mbwana, mwandishi wa maoni haya
Baada ya kutoa makala hiyo ambayo ni kolamu inayotoka katika gazeti hilo kila Jumapili, pia iliingia kwenye blog yangu kama utaratibu wangu.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Nasikitika kuona Serikali kwa kupitia Wizara ya Nishati na Madini chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakaanza kujibu kwa mtindo wa tangazo katika magazeti hapa nchini na kutumia fedha vibaya.
Ifikie wakati tuwe na huruma na fedha za Serikali. Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wanatumia gharama kubwa kujisafisha kwasababu ya makala yangu moja tu iliyosema Sera ya Umeme vijijini ipo kwenye makaratasi.
Gazeti la leo la Raia Mwema wametoa matangazo full page 2 kama ilivyokuwa kwa Mwananchi jana.
Hadi sasa ni dhahiri wametumia fedha zisizozidi Milioni 10 na sijui wataacha lini kutoa matangazo. Jana walikuwa Mwananchi, leo wamepewa Raia Mwema.

Ila najua bado magazeti mengine yenye nguvu, kama vile Tanzania Daima, Majira, Nipashe na Gazeti la Serikalai Habari leo.
Mbaya zaidi wanatoa matangazo mahali ambapo makala hiyo haijaandikwa wala haijasomwa? Kwanini? Huu ni utendaji kazi gani usiokuwa na huruma na Taifa letu? Fedha zinamwagika kiasi hiki?

Ningekuwa mimi Mkurugenzi REA, kama fedha kumbe za kuchezea zipo, ningenunua transfoma moja kwa ajili ya kijiji kimoja.

Kama lengo ni kuweka kumbukumbu sawa, ningeitisha mkutano na waandishi wa habari na kuwapa sera na mkakati wa kusambaza umeme vijijini hata kama nisipotaja jina la mwandishi wa makala hayo na gazeti lake.
Hatuwezi kuchezea fedha kijinga namna hii. Wadau hii kweli Haki? Usikose kusoma makala zangu katika Gazeti lako la Mtanzania kila siku. Hasa kwa makala ya Mgodi Unaotembea kila Jumatano na Jumapili.

No comments:

Post a Comment