Pages

Pages

Wednesday, December 19, 2012

Filamu zamuweka 'busy' Japhet Kaseba





Bingwa wa Kick Boxing, Japhet Kaseba akionyesha ubabe wake

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWANAMASUMBWI mahiri hapa nchini, Japhet Kaseba, amesema filamu zake mbili anazoandaa zinamuweka 'busy' kiasi cha kumfanya ashindwe kufanya mazoezi makali ya mapigano hadi hapo zitakapoingia sokoni.

Kaseba ambaye pia ni mahiri katika upande wa ngumi za meteke, maarufu kama Kick Boxing, anakamilisha filamu zake mbili ambazo ni Mafia na Dhambi ya Baba zinazotarajiwa kuingia sokoni mapema mwakani.

Akizungumza na Handeni Kwetu leo mchana, jijini Dar es Salaam, Kaseba alisema katika filamu hizo amewashirikisha wasanii wengi wenye uwezo na majina ya kutisha, akiwamo Kelvin, Mchumia Tumbo, Muhogo Mchungu na wengineo.

Alisema mara baada ya kumaliza programu za filamu zake hizo ikiwamo za studio, ataingia tena ulingoni, akianza na mazoezi kwa ajili ya kulinda jina na hadhi yake katika kona ya ngumi Tanzania, kama anavyojulikana na kuogopwa na wengi.

 “Filamu zinahitaji muda katika utengenezaji wake, hivyo ndio maana nimetingwa kwa shughuli za kazi zangu mbili ninazotarajia ziingie sokoni mapema mwakani, huku nikiamini kuwa zitakuwa moto wa kuotea mbali.

“Naamini wadau wote wataona makali yangu, hivyo mashabiki wasiogope kwa hatua hii kwakuwa zote ni kazi zangu na baada ya kumaliza hatua hii nitaingia tena katika kujiwinda kwenye masumbwi kama kawaida yangu,” alisema Kaseba.

Kaseba ni miongoni mwa mabondia wenye uwezo wa kutisha katika tasnia ya mchezo wa masumbwi kutokana na uwezo wake wa kurusha ngumi huku pia akiwahi kuwa bingwa wa Dunia wa Kick Boxing.

No comments:

Post a Comment