Pages

Pages

Tuesday, December 25, 2012

Penina atangaza utulivu na dini yake mpya


Penina huyo katika pozi

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MCHEZA filamu za kibongo Tanzania, Jenifer Raymond, maarufu kama Penina, amesema baada ya kubadili dini na kuwa Muislamu, ametulia na kuangalia zaidi maisha yake ya ndoa aliyofunga na mwarabu mmoja jina lake linahifadhiwa kwa sababu maalumu.
Penina akiwa na msanii mwenzake Mshindo Jumanne

Penina aliyewika zaidi katika sanaa, alitangaza kubadili dini hiyo kwasababu ya kutaka ndoa ya mwarabu mmoja.

Akizungumza na Handeni Kwetu mapema leo, Penina alisema aliamua kubadili dini kwa ridhaa yake akiwa na lengo la kuacha usichana wake.

Alisema katika maisha yake ya ndoa na mume wake huyo, ameweza kuvaa vyema uhusika wake, ingawa soko la sanaa bado analitendea, huku akiongeza kuwa u siri wa ndoa yao unatokana na kuogopa media zinavyoweza kuingilia kati na kuvuruga mapenzi ya watu.

Penina kama kawaida yake

“Nimeamua mwenyewe kubadili dini na kuolewa na mwarabu nikifuata dini yake ya Uislamu, lakini siri ilikubwa kubwa kwasababu bila hivyo ndoa yetu inaweza kuvunjika hasa kama wote tutakuwa wepesi kusoma na kuvifanyia kazi vichwa vya habari.

 “Naamini nimekuwa mtu mpya na mwenye majukumu ya kifamilia, hivyo maisha yetu yanaendelea kama kawaida, huku nikijiona mshindi kwa kuimudu siri hii ambayo wengi wao hawajawahi kuisikia na kuivumisha vibaya,” alisema Penina.

Penina alicheza filamu nyingi ikiwamo hiyo ya Penina aliyocheza na marahemu Steven Kanumba, Dar es Salaam na nyinginezo nyingi zilizompa umaarufu hapa nchini.

No comments:

Post a Comment