Pages

Pages

Tuesday, December 25, 2012

Tukiwekeza kwenye kilimo mambo yatakuwa poa

Kilimo cha kisasa ndicho kinachofaa zaidi kwa ajili ya kuwapatia wakulima faida katika kazi yao hiyo. Pichani ni bwawa la kuhifadhia yanayovunwa kutoka kwenye kisima kikubwa kwa ajili ya kusambaza kwenye njia za maji kwenye mashamba makubwa yanayowekezwa.

Kwa Tanzania kilimo cha aina hiyo kinafanywa zaidi na watu wenye nazo au makampuni makubwa, hivyo ili nchi iweze kupiga hatua, inabidi serikali kwa kushirikiana na taasisi za kilimo kuwasaidia angalau mikopo wakulima waliojiunganisha kwenye vikundi.

Kinyume cha hapo, sera ya kilimo kwanza, kilimo ni uti wa mgongo itaendelea kusemwa midomoni bila kuwa na mipango imara ya kuendeleza kwa ajili ya Taifa letu. Hatuwezi kuwa na uchumi imara kama sekta ya kilimo inasua sua.

Inawezekana, kila mmoja atimize wajibu wake.

No comments:

Post a Comment