Pages

Pages

Friday, December 21, 2012

Bundi atua tena Simba, mkutano waitishwa



Baadhi ya wanachama 698 waliotisha mkutano wa Simba, wakimsikiliza mwenyekiti wao wa muda, Dk Mohamedi Wande katikati aliyokaa karibu na Bi Hindu. Picha na Kambi Mbwana.
 
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BUNDI ametua tena katika klabu ya Simba, baada ya wanachama wanaofikia 698 kuitisha Mkutano wa Dharura uliopangwa kufanyika Travertine Hoteli, Desemba 30 mwaka huu, kwa ajili ya kujadili mambo yanayohusu timu yao.

Mkutano huo unafanyika wakati uongozi wa Simba, kupitia Mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage kutangaza kuwa wanaotangaza mkutano huo ni wahuni na hawawezi kumsumbua kwa njia yoyote.

Akizungumza mapema leo mchana, Mwenyekiti wa muda wa walioitisha mkutano huo, Mohamed Wandi, alisema kwamba wanachama wote wenye mapenzi mema na timu yao wanaombwa kufika kwa wingi.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage

Alisema timu yao inaendeshwa ovyo ovyo pamaja na kukanyagwa kwa Katiba yao iliyosababishwa wanaotaka mkutano huo kuitwa wahuni na uongozi wa Simba.

Ibara ya 22 kifungu cha 2 cha Simba SC kinasema kuwa wanachama hai waliofikia 500 wanaweza kuitisha mkutano wa dharura hasa kama Kamati ya Utendaji itashindwa kuitisha mkutano kama inavyohitajiwa na wanachama hao.

“Hii haiwezi kukubalika hata kidogo, maana mkutano wa dharura ni haki ya msingi kwa kila mwanachama ili mradi wawe wametimia wanachama 500, hivyo tayari tumezidi maana sasa wapo watu 698 wanotaka mkutano huo.

“Uamuzi utakaotolewa utakuwa wa haki na kusikilizwa na kila mtu, maana tayari uongozi hautaki kusikiliza madai yetu, hasa walipotaka mkutano kwa ajili ya kujipanga na ligi mzunguuko wa pili, usajili na namna gani ya kuiendeleza timu yetu na kuwa ya mfanao Barani Afrika,” alisema.

Kuitishwa upya kwa mkutano huo huenda kukawa moto mpya kwa Rage, hasa kama alijua wanachama hao wametulia, hasa walipokuwa wakisubiri siku zao 30 walizowapa uongozi kufikiria namna ya mkutano wao.

Katika hatua nyingine, wanachama wanaopenda kuhudhuria mkutano huo wanapaswa kulipia kadi zao kwa wale wanaodaiwa kutokukidhi vigezo vya kuwa wanachama, huku nakala za kuitisha mkutano huo zikisambazwa Kwa Msajili wa Vyama vya Michezo na vila Tanzania, TFF kwa kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Katiba, DRFA, IDRFA na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni.

No comments:

Post a Comment