Pages

Pages

Friday, December 21, 2012

Godbless Lema ashinda rufaa yake



 Godbless Lema

Na Mwandishi wa Handeni Kwetu
MWANASIASA machachari kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Godbless Lema, ameleta furaha mwisho wa mwaka kwa wafuasi na wanachama wao baada ya kushinda rufaa yake, mapema leo, hivyo kuwa nafasi ya kumuwezesha kuingia tena bungeni mwakani.

Habari zilizotufikia muda huu zinasema mwanasiasa huyo ameshinda na baadaye mwakani atawawakilisha tena wananchi wake katika kuliongoza Taifa hili kwa tiketi ya ubunge wa Arusha Mjini.

Rufaa hiyo ilitokana na Lema, aliyepinga kupokwa ubunge wake wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Wazee wa Peoples Power. Kushinda kwa rufaa hiyo kunasababisha mwanasiasa huyo kurejeshewa ubunge wake huo.

Hoja tatu ziliwalishwa katika jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, ili kuamua rufaa ya kesi ya mbunge huyo anayependwa na wengi, hasa katika maeneo ya Arusha na Vitongoji vyake.

Katika hukumu hiyo, kati ya hoja 18 zilizowasilishwa na upande wa rufaa kupinga hukumu hiyo, zipo hoja tatu zilizoonekana za msingi katika hukumu ya leo inayotolewa na majaji wanaosikiliza kesi hiyo hadi muda huu, ambao ni; Salum Massati, Bernard Luanda na kiongozi wao, Nathalia Kimaro.

Lema alivuliwa ubunge Aprili 5, 2012 katika hukumu iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalira, kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM; Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Baada ya hukumu hiyo iliyoumiza wana Chadema wengi, Lema, kupitia kwa Wakili wake, Method Kimomogoro alikata rufaa Mahakama ya Rufani na kuwasilisha hoja 18 za kupinga hukumu hiyo.

Kwa mtiririko wa hoja hizo, ya kwanza ni kama mpigakura anaweza kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi kwa niaba ya mgombea husika aliyeshindwa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi na nyinginezo zilizofanikisha Lema kurudishiwa Ubunge wake.

Habari zaidi juu ya kushinda kwa rufaa ya Lema tutaendelea kuwapatia kadri tutakavyoweza kuipata, huku tukiamini kuwa itakuwa ni karata turufu kwa wanazi, wanachama wote wa Chadema.

.

No comments:

Post a Comment