Pages

Pages

Friday, December 21, 2012

GFC Musica kutambulisha mmoja Krismasi



Repa wa bendi ya GFC (Modizo), akiwa jukwaani
 
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya muziki wa dansi ya GFC Musica ya mjini Morogoro, imeongeza mnenguaji wa kike aliyetajwa kwa jina la Flora Paschal  ambaye anatarajiwa kutambulishwa rasmi katika maonyesho ya sikukuu ya Krismasi na Boxing Day.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa bendi hiyo, Deogratius David 'Killer'
mnenguaji huyo amechukuliwa kutoka jijini Mbeya ingawa hakutaja kundi alichokuwa akifanyia kazi.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa Flora amechukuliwa ili kuziba nafasi
iliyoachwa na Samira aliyetimuliwa miezi mitatu iliyopita kutokana na na utovu wa nidhamu.

"Flora atatambulishwa rasmi kuanzia kwenye onyesho la mkesha wa
sikukuu ya Krisimasi pamoja na maonyesho mengine yatakayoendelea likiwemo la Boxing Day," alisema 'Killer'.

'Killer' alifafanua kuwa baada ya maonyesho hayo, mnenguaji huyo
atashiriki kikamilifu kwenye mazoezi ya maandalizi ya kushuti video ya nyimbo tatu ambazo ni miongoni mwa zile za albamu ya kwanza.

Alizitaja nyimbo hizo kuwa ni 'Jackpot Bingo', 'Mary', 'Marafiki
Wabaya' ambazo zimekuwa zikiporomoshwa kwenye maonyesho mbalimbali yanayofanywa na bendi hiyo mjini Morogoro.

GFC Musica ama Walugru Original kama inavyojiita, ilianza kazi rasmi mwanzoni mwa mwaka huu ikiwa na wanamuziki kama; Monica, Dk Steve, Rashid Katimba, Kuruthum Yusuph na Modizo (waimbaji).

Wengine ni Kalou Yambongo na Joel Kiame (solo), Kanuti (rythm),
Kibwana Magati na Eric Majaliwa (besi), Onesmo na Rogert (drums) na Fulangenge (tumba).

No comments:

Post a Comment